Thursday, December 20, 2012

MESSI ABWAGWA TUZO MWANAMICHEZO BORA WA ARGENTINA

ULIZA kikundi cha watu ni mtu gani wanaamini kuwa ndiye mwanamichezo bora duniani, jina la Lionel Messi ndilo utakalolisikia mara nyingi.
 
Isipokuwa kikundi hicho kikiwa kinaundwa na waandishi wa habari wa Argentina, ambao hawaoni kama Messi ni bora hata kwa nchini mwao tu. Wala nafasi ya pili wanaona hashiki.

Ila ni nafasi ya tatu aliyoshika nyota huyo wa Barcelona nyuma ya bondia Sergio Martinez na mpiganaji wa taekwondo, Sebastian Crismanich.


Pretty good year: Sergio Martinez with his trophy after beating Sebastian Chrismanich and Lionel Messi to the award
Sergio Martinez akiwa na tuzo yake baada ya kumshinda Sebastian Chrismanich na Lionel Messi 
Ready for it: Martinez will fight British boxer Martin Murray in April 2013
Niko tayari: Martinez atapambana na bondia wa Uingereza Martin Murray Aprili 2013

Mafanikio bab'kubwa aliyonayo Messi mwaka huu ya kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka 40 baada ya kufunga magoli 90 hadi sasa haikutosha kumpa tuzo hiyo.

Martinez alishinda taji la Olimpia de Oro baada ya kumchapa  Mmexico Julio Cesar Chavez Jr katika taji la ubingwa wa WBC mapema mwaka huu. Atapigana na bondia  Muingereza Martin Murray Aprili 2013.

What, not me? Lionel Messi finished third in the poll of Argentine journalists
What, not me? Lionel Messi amemaliza wa tatu katika tuzo ya waandishi wa habari ya mwanamichezo bora wa Argentina.

Crismanich, yeye, alikuwa mtu pekee wa Argentina aliyeshinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya London 2012.

"Ni heshima kubwa kushinda tuzo hii ambayo ilikuwa ikiwaniwa na wanamichezo kama Sebastian Crismanich na Leo Messi," Martinez alisema katika sherehe ya tuzo hizo Jumanne usiku.

Lakini kwa kuwa alishashinda tuzo hiyo ya Argentina mwaka 2011 na kwa kuwa anapewa nafasi kubwa zaidi ya kubeba kwa mara ya nne mfululizo tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia 2012, Messi hawezi kuwa amefadhaishwa sana.

No comments:

Post a Comment