Tuesday, December 18, 2012

BREAKING NEWZ........ MESSI AAFIKI MKATABA MPYA BARCELONA HADI MWAKA 2018

Messi

LIONEL Messi ameafiki mkataba mpya na Barcelona, utakaomweka kwa miamba hao wa Hispania hadi mwaka 2018.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina (25) amefurahia mwaka mzuri na klabu hiyo na timu yake ya taifa ambao amevunja rekodi, akifunga magoli 90 mwaka 2012.

Beki Carles Puyol (34), na kiungo Xavi Hernandez (32) pia wameafiki kusaini mikataba mipya itakayowaweka Barcelona hadi mwaka 2016.

"Katika wiki zijazo, Puyol, Xavi na Messi watasaini mikataba mipya," klabu hiyo imethibitisha.

Messi, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika Juni 2016, amekuwa katika kiwango cha kutisha mwaka huu.

Aliipita rekodi ya Gerd Mueller iliyodumu kwa miaka 40 ya kufunga magoli 85 katika mwaka mmoja wa kalenda wakati alipofunga magoli mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Betis Desemba 9.

Messi alifikisha jumla ya mabao yake mwaka 2012 kuwa 90 Jumapili kwa kufunga magoli mengine mawili wakati Barcelona ilipoifunga Atletico Madrid 4-1.

Ana nafasi ya kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia kwa mara ya nne mfululizo, kutokana na kujumuishwa katika orodha ya nyota watatu wanaoiwania pamoja na Cristiano Ronaldo na mchezaji mwenzake wa Barca, Andres Iniesta.

No comments:

Post a Comment