Monday, November 12, 2012

YOSSO WA TIMU B YA REAL MADRID AMUOKOA MOURINHO

Yosso wa timu B ya Real Madrid iitwayo Castilla, Álvaro Morata akishangilia goli lake baada ya kuifungia timu A goli la ushindi dhidi ya Levante jana usiku.

BAADA ya wiki mbili za utata kuhusu mfumo wa kupika vijana katika klabu ya Real Madrid, majibu yanaweza kuwa yamepatikana baada ya mchezaji wa timu ya Castilla (Madrid B), Álvaro Morata, kuingia kutokea benchi na kukiokoa kikosi cha Jose Mourinho kwa kufunga goli la ushindi la dakika za lala salama dhidi ya Levante jana katika ushindi wa 2-1.

Real Madrid waliondoka na pointi zote tatu lakini hali ya hewa ilikuwa ngumu katika uwanja uliojaa maji. Kikosi cha Mourinho kilicheza ovyo, lakini walifanya cha kutosha kuondoka na pointi zote.

Mvua na hali mbaya ya uwanja vilitawala vichwa vya habari wakati wa mapumziko, huku mpira ukikwama kwenye maji kila mara.

Licha ya uwanja mbaya, Real Madrid walipata goli la kuongoza katika dakika ya 20 kupitia kwa Cristiano Ronaldo. Mshmabuliaji huyo Mreno aliuwahi mpira wa 'fri-kiki' iliyopigwa na Xabi Alonso na kuukontroo kwa paja lake kabla ya kufumua shuti lililotinga wavuni.

Goli kutoka kwa Ángel katika dakika ya 62 liliwafanya wenyeji wapate matumaini ya kupata pointi na walitishia kuizamisha timu ya Mourinho.

Kuanzia wakati huo, Madrid walicharuka kusaka goli la ushindi, na Xavi Alonso alipoteza nafasi muhimu wakati penalti yake aliyopiga kupanguliwa na kipa wa Uruguay, Munúa.

Ilikuwa ni karata ya mwisho, na Mourinho akamgeukia Morata na kumpa nafasi. Ilionekana ni maamuzi sahihi, wakati Xabi alipogeuka kutoka "zero to hero" kwa kupiga "fri-kiki" babkubwa, na kumuacha yosso huyo akifunga kwa kichwa na kuwapa ushindi wa 2-1 katika dakika ya 85.

No comments:

Post a Comment