Tuesday, November 13, 2012

RVP AUMIA, AJITOA TIMU YA TAIFA UHOLANZI

Robin van Persie
 
ROTTERDAM, Uholanzi
TIMU ya taifa ya Uholanzi itaikabili Ujerumani kesho katika mechi ya kirafiki ya kimataifa bila ya mshambuliaji wao aliye katika kiwango cha juu Robin van Persie baada ya nyota huyo wa Manchester United kujitoa kikosini kutokana na maumivu ya paja.

Van Persie alicheza kwa dakika zote 90 katika mechi ambayo Man U ilishinda 3-2 ugenini dhidi ya Aston Villa Jumamosi, akimpikia Javier Hernandez goli la ushindi katika dakika ya 87 kwa 'fri-kiki' kali.

Mfungaji huyo wa magoli 31 katika mechi 71 za kimataifa anatarajiwa kuzibiwa pengo lake na mshambuliaji Klaas-Jan Huntelaar, ambaye anaichezea klabu ya Ujerumani ya Schalke 04 huku mwenye akiwa ameifungua Uholanzi magoli 34 katika mechi 59.

Kocha wa Uholanzi, Louis van Gaal atamkosa pia Wesley Sneijder katika mechi hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena. Sneijder bado anauguza maumivu ya paja na hajaichezea klabu yake ya Inter Milan tangu mwishoni mwa Septemba.

Van Gaal amewaita pia Jordy Clasie, Ruben Schaken, Stefan de Vrij, Jeroen Zoet na Bas Dost jana.

Ana kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Wajerumani ambao waliifunga Uholanzi 3-0 katika mechi ya kirafiki mwaka mmoja uliopita na pia walithibitisha wao ni bora kwao katika fainali za Euro 2012, baada ya kuwafunga 2-1 katika hatua ya makundi mjini Kharkiv.

No comments:

Post a Comment