Sunday, November 11, 2012

ONA JINSI MASHABIKI WA COASTAL UNION NA YANGA WANAVYOCHIMBIANA MKWARA JIJINI TANGA LEO... WAKATIZA MITAANI JIJINI TANGA KWA TAMBO NA VIJEMBE ... VIINGILIO MECHI YAO KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI VYAANDIKA REKODI... WATU WAANZA KUFURIKA UWANJANI KUANZIA SAA 7:00 MCHANA....!

Yanga leo hawatoki...! Shabiki maarufu wa klabu ya Coastal Union, Ibrahim 'Ibra' akionekana katika Barabara ya 8 jijini Tanga mchana huu baada ya kukamilisha michoro yake mwilini akiwachiomba mkwara Yanga kabla ya kwenda uwanjani kuishangilia timu yake itakayocheza jioni ya leo dhidi ya Yanga kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Novemba 11, 2012. 

Chezea Coastal wewe...! Shabiki Ibra wa Coastal akionyesha mchoro wake kwa mbele kuipiga mkwara Yanga kabla ya mechi yao ya leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Hapa ni katika Barabara ya 8 jijini Tanga mchana huu Novemba 11, 2012.
Mashabiki wa Yanga wakiandamana na vigoma na vuvuzela katikam maeneo ya stendi kuu ya mabasi jijini Tanga leo ikiwa ni mikwara yao kabla ya kuwavaa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jioni.

Mashabiki wa Tawi la Mpira Mipango kutoka Keko, Temeke jijini Dar es Salaam wakiungana na wenzao wa Tanga kuzunguka mitaa ya jiji hilo leo kabla ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani leo jioni Novemba 11, 2012.

Coastal leo hawatoki... ! Mashabiki wa Yanga wakiendelea kuzunguka katika mitaa mbalimbali ya jiji la Tanga wakianzia katika stendi kuu ya mabasi mchana huu kabla ya mechi yao ya jioni dhidi ya wenyeji Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Novemba 11, 2012.
Mechi kali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayokuwa ya kumalizia mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kati ya wenyeji Coastal Union na Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo jioni imeandika rekodi baad ya tiketi zake kuuzwa kwa bei 'mbaya' kuliko mechi zote za msimu huu ikiwamo ya mabingwa watetezi, Simba dhidi ya wenyeji hao (Coastal).

Mauzo ya tiketi hizo leo ni Sh. 5,000 kwa kiingilio cha chini (ambazo kufikia saa 9:00 watu walikuwa wakizilangua kwa Sh. 7,000), Sh. 10,000 na Sh. 15,000 kwa kiingilio cha juu wakati katika mechi nyingine zenye mvuto zaidi ikiwamo ya Simba dhidi ya Coastal, viingilio vilikuwa Sh. 4,000, Sh. 7,000 na Sh. 10,000.

Licha ya viingilio hivyo vikubwa, mashabiki walionekana wakichangamkia tiketi hizo kwa wingi, wengine wakitokea jijini Dar es Salaam na baadhi katika maeneo ya jirani ya jiji la Tanga kama Kabuku, Mwakidila, Duga Maforoni, Pangani, Muheza, Korogwe na kwingineko.

No comments:

Post a Comment