Saturday, November 3, 2012

VAN MAGOLI AISAIDIA MAN UNITED KUUA NDUGU ZAKE WA ZAMANI ARSENAL

Goooooooo!..... Chezea RVP wewe?... Straika wa Manchester United, Robin van Persie (kulia) akishuti kufunga dhidi ya beki na nahodha wa Arsenal, Thomas Vermaelen wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester leo. Man U ilishinda 2-1 kupitia magoli ya Van Persie na Evra wakati la Arsenal lilifungwa na Santi Cazorla. Picha: REUTERS
Van Magoli akitupia bao lake la 10 msimu huu akiwa na Man United.
Ngoma ngumu... Kocha Arsene Wenger akiwa hoi wakati jahazi lake likizama Old Trafford leo
Mimacho kodooo.....sijui niache kazi?
Rooney (kushoto) akijialaumu baada ya kukosa penalti
RVP akijilaumu baada ya kupoteza nafasi
Wachezaji wa Arsenal, Per Mertesacker (kushoto na Olivier Giroud wakirukia mpira wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester leo.
Kiungo majeruhi wa Manchester United, Shinji Kagawa (kulia) akishuhudia mechi pamoja na wachezaji wenzake kutokea jukwaani wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester leo. Picha: REUTERS
Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla (kulia) akimlalamikia refa Mike Dean baada ya kuwapa Manchester United penalti wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester leo.
Straika wa Manchester United, Wayne Rooney (kulia) akiliwazwa na mchezaji mwenzake Robin van Persie baada ya kukosa penalti wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester leo. Picha: REUTERS
Mchezaji wa Swansea City, Leon Britton (kushoto) akiwania mpira dhidi ya kiungo wa Chelsea, Oscar wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Liberty mjini Swansea, Wales Kusini, leo Novemba 3, 2012. Timu hizo zilitoka 1-1. Picha: REUTERS
 
Mchezaji wa Swansea City, Ki Sung-Yeung akiwania mpira dhidi ya straika wa Chelsea, Fernando Torres wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Liberty mjini Swansea, Wales Kusini, leo Novemba 3, 2012. Timu hizo zilitoka 1-1. Picha: REUTERS

Mchezaji wa Wigan Athletic, Ben Watson (wa pili kulia) akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Tottenham Hotspur wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa White Hart Lane mjini London leo Novemba 3, 2012. Picha: REUTERS
Kipa wa Tottenham Hotspur, Brad Friedel akishndwa kuzuia mpira usivuke mstari wa goli wakati mchezaji wa Wigan Athletic, Ben Watson akifunga wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa White Hart Lane mjini London leo Novemba 3, 2012. Picha: REUTERS

LONDON, England
ROBIN van Persie alifunga dhidi ya klabu yake ya zamani wakati Manchester United ilipoifunga Arsenal iliyobakiwa na wachezaji 10 uwanjani magoli 2-1 yaliyowapeleka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England leo jioni, huku Chelsea wakilshikiliwa kwa sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Swansea City.

Mholanzi huyo aliye katika kiwango cha juu, ambaye alijiunga na Man United akitokea Arsenal Agosti akiwa ameifungia Gunners magoli 37 ya ligi msimu uliopita, alihitaji pungufu ya dakika tatu kuwafungia wenyeji goli la kuongoza kufuatia makosa ya beki Thomas Vermaelen na Patrice Evra akakamilisha ushindi wa kujiamini kwa kichwa katika dakika 67.

Santi Cazorla alifunga goli la dakika za majeruhi kwa timu iliyofadhaisha ya Arsenal, ambayo ilibakiwa na wachezaji 10 baada ya mapumziko wakati kiungo aliyerejea kutokea kuwa majeruhi wa zaidi ya mwaka nje ya uwanja Jack Wilshere kutolewa kwa kadi ya pili ya njano.

Wayne Rooney pia alikosa penalti kwa Man United kabla ya mapumziko lakini hapakuwa na muda wowote ambao ilionekana kama makosa yake yangeigharimu timu.

Man United wana pointi 24 kutokana na mechi 10 na wamebaki kileleni baada ya Chelsea kufikisha pointi 23 kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Swansea City. Goli la Chelsea lilifungwa na Victor Moses kwa kichwa kabla ya wenyeji kusawazisha katika dakika 87.

Mabingwa Manchester City, ni wa tatu wakiwa na pointi 21, watakamilisha siku ya leo kwa kucheza dhidi ya West Ham United (saa 2:30 usiku).

Arsenal walilala 8-2 uwanjani hapo msimu uliopita na huku wakiwa hawaonekani kuwa hatarini kula kipigo kama kile tena, matokeo ya mwisho yalikuwa ni ya kushukuru kwa kikosi cha Arsene Wenger.

Bila ya magoli ya Van Persie, wameonekana hawana makali katika ligi msimu huu na kikosi hicho cha Wenger tayari kimeshaanza kuaga mbio za ubingwa mapema, kikiwa na pointi 15 katika mechi 10.

Na akawa Van Persie wa kuwadhuru.

Ni mara chache sana huhitaji msaada wowote ili kufunga lakini mchezaji mwenzake wa zamani Vermaelen alimwezesha kufunga katika dakika ya tatu wakati alipojaribu kuosha krosi ya Rafael na mpira ukatua miguuni mwa Van Persie ambaye aliunganisha moja kwa moja Vito Mannone.

"Siku spesho, mwisho ilikuwa mechi nzuri," Van Persie, ambaye hakushangilia goli lake, aliiambuia Sky Sports.

"Ujumbe unajieleza wenyewe (kwanini sikushangilia). Nimecheza miaka nane pale na nilikuwa na kipindi kizuri. Nilitaka kuwaheshimu mashabiki, kocha na klabu yote."

Arsenal ilishindwa kuleta tishio lolote na Wilshere, ambaye alianza kwa mara ya pili tu tangu aliporejea kutokea kuwa majeruhi wa muda mrefu, hakuonyesha chochote cha maana - akipata kadi ya njani kwa kumchezea Tom Cleverly.

Van Persie alipoga shuti jingine ambalo liliokolewa na Mannone wakati  Man United wakisaka goli la pili na muda mfupi kabla ya mapumziko wenyeji walipewa penalti wakati shuti la Ashley Young lilipozuiwa kwa mkono wa Cazorla na refa Mike Dean akaonyesha kisanduku ya penalti.

Arsenal walifurahia makosa ya Rooney ambaye penalti yake ililenga chini ya nguzo ya kulia ya lango la Mannone.

Vermaelen alifanya kosa jingine baya baada ya mapumziko, akimuachia mpira Van Persie ambaye krosi yake ya chini ikionekana kumualika Antonio Valencia lakini alishindwa kuugusa mbele ya lango.

Evra mwishowe aliwapa Man United muda wa kupumua wakati alipofunga kwa kichwa katika dakika ya 67, dakika mbili kabla ya Wilshere kuonyeshwa kadi ya pili ya njanokwa kumkanyaga vibaya Evra.

Cazorla aliwapa mashabiki wa Arsenal kitu cha kushangilia, akipiga shuti la upinde wa mvua lililokwenda moja kwa moja wavuni katika shuti la mwisho la mechi.

No comments:

Post a Comment