Wednesday, November 28, 2012

THEO WALCOTT, BAKARY SAGNA WATOSWA KATIKA KALENDA MPYA YA ARSENAL YA MWAKA UJAO 2013


Theo Walcott

Bacary Sagna
LONDON, England
KLABU ya Arsenal imemuacha straika Theo Walcott aliye katika mvutano na timu hiyo kuhusiana na mkataba wake mpya kwenye kalenda yao ya mwaka 2013, imefahamika.

Gazeti la The Sun limesema vilevile kuwa Bacary Sagna, ambaye pia anaisumbua klabu hiyo katika mazungumzo yao kuhusu kusaini mkataba mpya, ni mchezaji mwingine nyota aliyeachwa katika kalenda rasmi ya timu hiyo kwa mwaka ujao.

Walcott (23), haonekani kokote katika toleo la kalenda hiyo ya mwakani baada kushindwa kuwahakikishia kwamba atabaki klabuni hapo.

Straika huyo wa kimataifa wa England, ambaye hivi sasa anapokea mshahara wa paundi za England 65,000 kwa wiki katika mkataba utakaomalizika Juni, alikataa ofa aliyopewa y kusaini mkataba mpya utakaombatana na mshahara wa paundi za England 80,000 kwa wiki.

Mgomo wake huo tayari umeziamsha klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England zikiwamo za Liverpool na Manchester City, ambao wanaaminika kuwa wako tayari kuilipa Arsenal paundi za England milioni 15 ili kumnasa wakati wa kipindi cha uhamisho wa dirisha dogo la Januari.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema wazi kwamba anataka na anatarajia kwamba Walcott atasaini mkataba mpya wa kumbakiza katika klabu yao.

Hata hivyo, wengi wanaamini kwamba sasa Arsenal wameshakubali kumpoteza Walcott baada ya litomjumuisha katika kalenda yao mpya ya mwaka 2013, ingawa Wenger amedai kwamba kuachwa katika kalenda si ishara kwamba nyota hao watapigwa bei.

No comments:

Post a Comment