Wednesday, November 28, 2012

DI MARÍA, CALLEJON WATUPIA MABAO NA KUIPA REAL MADRID ILIYOCHEZESHA VITOTO USHINDI WA 3-0 DHIDI YA ALCOYON… SASA WASONGA MBELE KOMBE LA MFALME



Di Maria akifunga goli dhidi ya  Alcoyano katika mechi yao ya Kombe la Mfalme kwenye Uwanja wa Real Madrid jana usiku.
MADRID, Hispania
Kikosi kilichojaa yosso cha Real Madrid kilifuzu kwa hatua inayofuata ya michuano ya Kombe la Mfalme baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Alcoyano katika mechi isiyokuwa na matukio ya kusisimua usiku wa kuamkia leo.

Magoli ya Real yalipatikana kuelekea mwishoni mwa mechi ambapo habari mbaya kwa washindi ni jeraha la 'enka' alilopata beki wa kati,  Raúl Albiol ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kuanza kwa mechi.

Katika dakika ya 72, Di María alitumia vyema pasi ya Karim Benzema ndani ya boksi la michuano ya Kombe la Mfalme baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Alcoyano kuipa Real Madrid goli la utangulizi, huku ikijua vilevile kuwa tayari walishakuwa mbele kutokana na ushindi wa 4-1 walioupata katika mechi yao ya kwanza.

Callejón alifanya ubao wa magoli usomeke 2-0 katika dakika ya 88 baada ya kutumia vyema pasi 'kali' kutoka kwa Özil na kuitumia vyema kwa kupiga shuti lililokwenda wavuni katika dakika ya 91.

Raúl Albiol alicheza kwa mara ya kwanza akiwa nahodha wa Real Madrid, alidumu na kitambaa cha uongozi wa timu yake kwa dakika moja tu kabla hajaumia 'enka'. Beki huyo wa kati wa timu ya taifa ya Hispania alilazimika kutoka na kukabidhi madaraka yake kwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno, Fabio Coentrao.

Denis Cheryshev, hata hivyo, aliandika historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Urusi kuwahi kupangwa katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid. Amekuwa mchezaji wa 16 kutoka katika timu ya vijana ya Real kupata nafasi ya kucheza mechi za mashindano chini ya utawala wa kocha José Mourinho.

Mou aliwapanga wachezaji sita kutoka shule ya soka ya Real Madrid katika katika kikosi chake cha kwanza: Adán, Nacho, José Rodríguez, Cheryshev, Callejón na Morata.

No comments:

Post a Comment