Wednesday, November 28, 2012

TAZAMA JENEZA LA SHAROMILIONEA NA KABURI LAKE LINAVYOONEKANA KABLA YAKUZIKWA LEO... MZEE MAJUTO APATA NAFUU... NAYE ASHIRIKI MAZISHI MWANZO-MWISHO!

Jeneza la Sharomilionea likipelekwa msikitini kwa ajili ya kuswaliwa mchana huu, leo Novemba 28, 2012.

Kaburi la marehemu Sharomilionea linavyoonekana karibu na nyumba yao kabla ya mwili wake kuzikwa humo leo mchana (Novemba 28, 2012)  kijijini kwao Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

Marehemu Sharomilinea enzi za uhai wake.
Hatimaye mwili wa msanii Hussein Mkitei 'Sharomilionea' uliondolewa kutoka katika Hospitali Teule ya Muheza, ukaoshwa na kuwekwa kwenye jeneza kabla ya kuswaliwa na kuelekea kuzikwa katika kaburi lililochimbwa karibu na nyumba yao, kwenye kijiji cha Lusanga, wilaya ya Muheza mkoani Tanga mchana huu.

Taarifa zaidi zimedai kuwa mshirika wa marehemu Sharomilionea katika uigizaji, Mzee King Majuto, alipata nafuu baada ya kuwa katika hali mbaya kutokana na mshituko uliompata kwa kifo cha Sharomilionea na kwamba leo, alikuwa ni miongoni mwa maelfu ya watu waliokuwa kwenye mazisi ya msanii huyo.

Sharomilionea alifariki dunia juzi mishale ya saa 3:00 usiku baada ya gari alilokuwa akiliendesha aina ya Toyota Harrier kupata ajali mbaya iliyomuua papo hapo wakati akikaribia kijijini kwao Lusanga ili kwenda kuwajulia hali wazazi wake.

Wasanii mbalimbali nyota, viongozi wa siasa na serikali ni miongoni mwa watu kibao waliojitokeza kumzika Sharomilionea mchana huu.
 

No comments:

Post a Comment