Wednesday, November 21, 2012

TAZAMA ORODHA YA MAKOCHA WANAOPEWA NAFASI KUBWA YA KUMRITHI ROBERTO DI MATTEO ALIYETIMULIWA CHELSEA... WAMO VINARA RAFA BENITEZ, PEP GUARDIOLA, HARRY REDKNAPP, JOSE MOURINHO, ZOLA, JOHN TERRY!

Kula shavu mwana...! Pep Guardiola na binti yake Maria wakikatiza katika mitaa ya jiji la New York, Marekani Oktoba 16, 2012. Kocha huyu wa zamani wa Barcelona ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Di Matteo katika klabu ya Chelsea.

LONDON, England
Baada ya kocha Roberto Di Matteo kutimuliwa leo katika klabu ya Chelsea kufuatia kipigo cha 3-0 walichokipata jana kutoka Juventus katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, makocha kadhaa wametajwa kuwa na uwezekano wa kurithi mikoba katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Englan.

Miongoni mwao, kocha wa zamani wa Liverpool na Inter Milan anapewa nafasi kubwa ya kutwaa nafasi hiyo, akifuatiwa na Mhispania mwenzake aliyekuwa akiifundisha Barclona, Pep Guardiola na pia kocha wa zamani wa klabu ya Tottenham Hottpurs, Harry Redknapp.

Fuatilia orodha hiyo iliyotolewa mchana huu kwa mujibu wa wacheza kamari wa Skybet.

Rafael Benitez 4/6

Pep Guardiola 3/1

Harry Redknapp 5/1

Avram Grant 12/1

Gianfranco Zola 16/1

Andriy Shevchenko 20/1

Steve Clarke 20/1

Jose Mourinho 25/1

David Moyes 28/1

John Terry 33/1

Dan Petrescu 40/1

David Beckham 50/1

No comments:

Post a Comment