Wednesday, November 21, 2012

RONALDO KAMWE HATAKUJA KUWA BORA KAMA MESSI - TEVEZ

Tevez akishangilia goli la tatu la Machester City alilofunga kwa penalti dhidi ya Aston Villa katika mechi yao ya Ligi ya Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad Novemba 17, 2012.Man City walishinda 3-0.
Tevez (kulia) akipongezwa na Silva wakati akishangilia goli la tatu la Machester City alilofunga kwa penalti dhidi ya Aston Villa katika mechi yao ya Ligi ya Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad Novemba 17, 2012.Man City walishinda 3-0.

Cristiano Ronaldo
Lionel Messi

CARLOS Tevez amemweleza Cristiano Ronaldo kwamba kamwe hatakuja kuwa mchezaji bora kama Lionel Messi.

Ronaldo amerejea mjini Manchester leo kuisaidia Real Madrid kuisukuma Manchester City nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.


Mreno huyo anatarajiwa kuwa nyota katika mechi yao ya leo usiku usiku ya Kundi D kwenye Uwanja wa Etihad. 


Ronaldo amekuwa katika kiwango kizuri tangu alipoondoka Manchester United na kujiunga na Real mwaka 2009 kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 80, akifunga magoli 124 katika mechi 113 tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Hispania.


Mjadala wa nani ndiye mchezaji bora duniani unaendelea kuwa mkali, huku maoni yakiwaangukia Ronaldo na Messi.


Tevez alisema: “Cristiano ni mmoja wa wachezaji bora duniani. Nadhani unapaswa kujaribu na kuhakikisha hakutangulii. Akipata nafasi ya kukutangulia, ni hatari sana na anapiga mashuti vizuri, hivyo unapaswa kujaribu na kumzuia mbali na lango.


"Nadhani ni haki yake Cristiano kuamini kwamba yeye ni bora duniani. Mtu yeyote anayefunga magoli 37 hadi 40 kwa msimu anayo haki ya kuamini hivyo, lakini ukinisukuma mimi, daima nitaenda upande wa Messi."


Messi jana usiku alifunga magoli mawili katika ushindi wa 3-0 wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kufikisha jumla ya mabao 80 katika mwaka huu wa 2012, na sasa amebakisha magoli matano tu kuifikia rekodi ya muda wote ya kufunga magoli mengi zaidi katika mwaka mmoja wa kalenda inayoshikiliwa na Mjerumani Gerd Muller aliyefunga magoli 85 mwaka 1972.

No comments:

Post a Comment