Monday, November 19, 2012

TANESCO YATINGA MAHAKAMA YA RUFAA TANZANIA KUPINGA HUKUMU YA KUWATAKA WAILIPE KAMPUNI YA DOWANS SHILINGI BILIONI 94... WAPINGA KWA KUDAI KWAMBA WAKILIPA 'MIHELA' HIYO WATAYUMBA NA KUPATA HASARA KUBWA...!

Mitambo ya kufua umeme ya Dowans.
Hatimaye Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetinga katika Mahakama ya Rufaa kutaka zuio la utekelezaji wa hukumu iliyowataka wailipe Kampuni ya Kufua Umeme ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Limited jumla ya Sh. bilioni 94 na sasa rufaa hiyo itaanza kusikilizwa tarehe 5 ya mwezi ujao.

TANESCO ambao rufaa yao hiyo imesajiliwa kwa namba 142 na kupangwa kusikilizwa mbele ya jopo la majaji Katheline Uriyo, Natalia Kimaro na Bernard Luanda, wamedai kupitia hati ya maombi yao kuwa .

Kupitia hati ya maombi yao, Tanesco wanadai kuwa wanapinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam uliokazia tuzo iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) iliyowaamuru kuilipa Dowans mabilioni hayo ya fedha.

TANESCO wamedai kuwa Sh bilioni 94 walizoamuriwa kuilipa Dowans ni kiasi kikubwa na kwamba, wakitekeleza amri hiyo, watayumba kiuchumi na kupata hasara kubwa.


 TANESCO imedai kuwa baada ya kuamriwa na ICC kulipa tuzo hiyo, tayari wameshalipa dola za Marekani milioni 30 kama dhamana kutokana na amri iliyotolewa na mahakama hiyo.

Mahakama ya biashara ya kimataifa iliiamuru TANESCO kuilipa Dowans dola za Marekani 68,812,630. Tuzo hiyo iliyotolewa Novemba 15, 2011  ilisajiliwa na kusikilizwa mbele ya Jaji Emilian Mushi wa Mahakam Kuu ambaye baadaye alikazia hukumu ya kuitaka TANESCO ilipe mara moja fedha.

No comments:

Post a Comment