Tuesday, November 20, 2012

FERNANDO TORRES ACHOSHWA NA UKAME WA MABAO CHELSEA... SASA YUKO TAYARI KURUDI HISPANIA KATIKA KLABU YAKE YA ZAMANI YA ATLETICO MADRID...FALCAO ADAIWA YU MBIONI KUMRITHI CHELSEA!

Fernando Torres
LONDON, England
Straika wa Chelsea, Fernando Torres amechoshwa na ukame wa mabao unaomuandama katika Ligi Kuu ya England tangu ahamie Chelsea na sasa anataka kuihama timu yake hiyo iliyomnunua kwa paundi za England milioni 50 (Sh. bilioni 130) kutoka Liverpool ili arejee kwao Hispania.

Gazeti la Daily Mail limesema kuwa kifikra, Torres anawazia kurudi Hispania wakati akiangalia uwezekano wa kurudi katika kiwango chake cha awali kilichomfanya awe straika wa kuogopwa duniani kote.

Wazo kwamba wasifu wake umekuwa ukiporomoka tangu atue Chelsea limekuwa likimsumbua straika huyo wa zamani wa Liverpool, lakini inaelezwa kwamba binafsi amekubali kuwa ni lazima aondoke London magharibi, huku Hispania kukiwa mahala sahihi kwa kwenda.

Kadri inavyoonekana, Torres anaweza kurudi katika klabu yake ya Atletico Madrid na kuwa sehemu ya makubaliano ya ya kumleta Chelsea straika nyota wa sasa wa Atletico, Mcolombia Radamel Falcao.

No comments:

Post a Comment