Monday, November 19, 2012

WASANII WALIONG'ARISHA TAMASHA LA TUZO ZA AMERICAN MUSIC AWARDS JANA

Rapa Nicki Minaj akishukuru kwa tuzo ya Msanii Bora wa Rap/Hip-Hop wakati wa tamasha la 40 la tuzo za muziki la American Music Awards kwenye Ukumbi wa Nokia Theatre mjini Los Angeles, California, Marekani juzi Novemba 18, 2012.
Muimbaji Justin Bieber akishukuru kwa tuzo Msanii Bora wa Kiume wa Pop/Rock wakati wa tamasha la 40 la tuzo za muziki la American Music Awards kwenye Ukumbi wa Nokia Theatre mjini Los Angeles, California, Marekani jana Novemba 18, 2012. Justin Bieber alishinda tuzo ya kwanza ya usiku wa jana huku akiwa amezungukwa na utata wa mahusiano yake ya kimapenzi yaliyoyumba na kimwana Selena Gomez. Wakati akipokea tuzo hiyo alisema, "Hii ni kwa wenye chuki."

Justin Bieber akipigwa busu la kustukizwa na mchekeshaji Jenny McCarthy wakati akipokea tuzo ya Albamu Bora ya Pop/Rock kupitia albamu yake ya Believe

No comments:

Post a Comment