Wednesday, November 7, 2012

PICHA YA OBAMA AKIMKUMBATIA MKEWE KAMPENI ZA UCHAGUZI YAVUNJA REKODI KWENYE TWITTER... YARUSHWA MARA NUSU MILIONI NA KUVUNJA REKODI YA AWALI ILIYOKUWA IKISHIKILIWA NA JUSTIN BIEBER....!

Mmmmmhhh...!

Obama akisalimiana na Justin Bieber
Obama na mkewe (kushoto) na kulia ni aliyekuwa mpinzani wake wakati wa uchaguzi, Mitt Romney na mkewe
Picha ya Rais wa Marekani, Barack Obama akimkumbatia mkewe Michelle Obama ambayo ilipostiwa katika kampeni za rais huyo jana usiku ilivunja rekodi kwa kurushwa tena mara zaidi ya nusu milioni.

Picha hiyo ilipostiwa muda mfupi kabla Obama hajatabiriwa kushinda kupitia mitandao mbalimbali -- taarifa zilizoambatana na picha yenye maelezo yasemayo, "Miaka minne zaidi."

Kwa mujibu wa AllTwitter.com, rekodi ya awali katika kurasa za mtandao wa kijamii wa Twitter kabla ya Jumanne ilikuwa ikishikiliwa na ujumbe wa msanii nyota wa muziki wa pop, Justin Bieber, aliokuwa akimuomboleza Avalanna Routh, shabiki wake wa miaka sita aliyekufa kwa maradhi ya kansa.

No comments:

Post a Comment