Wednesday, November 14, 2012

PELE AKIMBIZIWA HOSPITALI... KUPASULIWA NYONGA


SAO PAULO, Brazil
Gwiji wa soka wa Brazil, Edson Arantes do Nascimento, a.k.a Pelé, sasa akiwa na miaka 72, amelazwa kwenye Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo.

Msemaji wa hospitali hiyo amethibitisha kwamba Pelé alikuwa akitibiwa kwenye kituo chao, lakini hakutaka kueleza kwa undani zaidi akihofia kuingilia masuala binafsi ya famiia ya nyota huyo wa zamani wa Brazil.

Gazeti la Brazil, 'Folha de Sao Paulo', likikariri chanzo kimoja kisichotajwa lakini kilicho karibu na Pelé, limedai kwamba mfalme huyo wa soka ulimwenguni amefanyiwa upasuaji wa nyonga.

No comments:

Post a Comment