| Mashabiki wa Yanga walivyokuwa wakionekana kwenye mitaa ya jiji la Tanga kabla ya mechi yao dhidi ya Copastal Union ambayo Yanga walishionda 2-0. |
| Mashabiki wa Yanga wakiwa katika eneo la stendi kuu ya mabasi jijini Tanga |
| Mashabiki wengine jijini Tanga walitupia jezi za Yanga kumtania mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage kama huyu anayeonekana kushoto. |
| Hapa waligongana mashabiki wa Yanga na Coastal katika eneo la Stendi Kuu ya mabasi jijini Tanga. |
| Mashabiki Yanga wakitamba na ngoma zao. |
| Ilikuwa ni burudani ya aina yake jijini Tanga wakati mashabiki wakiendeleza vijembe kabla ya mechi kati ya Yanga na Coastal Union. Yanga ilishinda 2-0. |
| Ni ngoma na vuvuzela kwa kwenda mbele. |
| Mashabiki wengine walisafiri kwa mabasi kutoka jijini Dar es Salaam hadi jijini Tanga kuishangilia timu yao. Hawa ni Wazee wa Mipango kutoka Keko, Temeke. |
| Baadhi ya mashabikii wa Yaga wakipata msosi kabla ya kwenda uwanjani kuishangilia timu yao. |
| Mashabiki walikuwa wametapakaa katika mitaa mingi jijini Tanga kabla ya pambano la Yanga dhidi ya wenyeji Coasta. |
| Hapa kulikuwa na mchangayiko wa mashabiki wa Yanga na Coastala. |
| Hapa sasa nbi nje ya Uwanja wa Mkwakwani... mashabiki wakiwa mbioni kuingia uwanjani kushuhudia mechi ya Yanga dhidi ya wenyeji Coastal Union. |
| Yanga tutashinda 3-0...! Ndivyo shabiki huyu alivyokuwa akitabiri kabla ya kuanza kwa mechi yao dhidi ya Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Hata hivyo, Yanga walishinda 2-0. |
| Kama kawa jijini Tanga... mashabiki wengi walifika kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakiwa na baiskeli. |
| Mgambo JKT pia walikuwapo... hili ndilo basi lao lililowaleta uwanjani. |
| Eneo hili walijaa mashabikji wa Yanga... ilikuwa ukionekana na jezi ya rangi nyekundu na nyeupe ya Coastal umeondolewa kwa kubebwa juujuu! |
| Eneo hili walijaa mashabikji wa Coastal... ilikuwa ukionekana na jezi ya rangi ya njano na kijani ya Yanga; umeondolewa kwa kubebwa msobemsobe! |
No comments:
Post a Comment