Tuesday, November 13, 2012

NAVARRO: BEKI MCHEZA RAFU ALIYEMPIGA KIWIKO RONALDO, KUMKITA KWA NJUMU FIGO NA KUMTIMBA KWENYE ENKA LIONEL MESSI... ALIWAHI PIA KUMPIGA NGUMI YA USO BURDISSO WA INTER NA KUMVUNJA PUA

Masikini jembe.... Ronaldo akivuja damu baada ya kupigwa kiwiko na David Navarro

Muunganiko wa picha zinazoonyesha tukio la Ronaldo kujeruhiwa. Kushoto akipigwa kiwiko na Navarro, katikati akimwagika damu na na kulia akishonwa pembeni ya uwanja wakati wa mechi yao dhidi ya Levante juzi Jumapili. Real Walishinda 2-1.
Matukio tofauti yanayoonyesha uchezaji usio wa kiungwana wa David Navarro. Juu kulia akimpiga ngumi ya uso Nicolas Burdisso iliyomvunja pua

Damu zilimmwagika Ronaldo kama bomba...
Ronaldo alivyo sasa baada ya kushonwa
David Navarro
David Navarro

BEKI mtukutu wa Levante, David Navarro amesema hakudhamiria kumuumiza Cristiano Ronaldo baada ya kumpiga kiwiko cha usoni mshambuliaji huyo wa Real Madrid na kumchana vibaya juu ya jicho la kushoto waliporuka kuwania mpira wa kichwa wakati wa mechi yao ya La Liga juzi Jumapili.

Ronaldo awali alicheza baada ya kutibiwa pembeni ya uwanja na akafunga goli la kuongoza la Real katika dakika ya 21 katika mechi hiyo waliyoshinda 2-1. Lakini alilazimika kupumzishwa wakati wa mapumziko baada ya kupata tatizo la kuona vizuri.


"Ilikuwa ni ajali, hamna wakati wowote niliojaribu kumuumiza Cristiano Ronaldo," Navarro, ambaye ana historia ya ukorofi, alisema katika tovuti ya Levante (www.levanteud.com).


"Kuna mambo yanatokea mchezoni na nayajutia kwa sababu nimemjeruhi, lakini narudia kwamba ni jambo ambalo sikudhamiria kulifanya," alisema beki huyo mwenye umri wa miaka 32.


Navarro aliwasiliana na Ronaldo Jumatatu kumjulia hali na kumtakia apone haraka, Levante ilisema.


Vyombo vya habari vya Hispania jana Jumatatu vilionyesha video za matukio ya nyuma yanayomuhusisha Navarro, likiwamo la vurugu ya wachezaji wengi wakati wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baina klabu yake ya zamani ya Valencia na Inter Milan Machi 2007.


Navarro alimpiga ngumi kiungo wa Inter, Nicolas Burdisso usoni, akamvunja pua, na akafungiwa na UEFA kucheza soka kwa miezi saba.


Matukio mengine yanajumuisha tukio la kutisha la kumrukia kiungo wa zamani wa Real Madrid, Luis Figo huku akiwa amemuinulia njumu mbele wakati wa kuwania mpira na pia kumtimba mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi kwenye 'enka'.


Ronaldo atakosa mechi ya kirafiki ya Ureno ugenini Gabon kesho kutokana na majeraha hayo, shirikisho la soka la nchi yake (FPF) lilisema jana Jumatatu.

No comments:

Post a Comment