Friday, November 30, 2012

MICHAEL ESSIEN AONDOKA REAL MADRID NA KURUDI CHELSEA AKATIBIWE... AVAA JEZI YAKE NA. 5 CHELSEA

Nimerudi...! Essien (katikati) akiwa klabuni Chelsea jijini London jana.
Karibu mwana...! Essie (kulia) akiwa na washkaji zake wa long taim kitambo klabuni Chelsea; Ashley Cole (katikati) na nahodha John Terry.
LONDON, England
Michael Essien ameamua kurudi katika klabu yake ya Chelsea akitokea Real Madrid anakocheza kwa mkopo, lengo likiwa ni kwenda kutibiwa jeraha lililomuweka nje ya uwanja tangu Novemba 11.

Kiungo huyo amekuwa katika jiji la London tangu wiki iliyopitakupata matibabu kutoka kwa madaktari wa Chelsea, ambao wanamjua vizuri zaidi mchezaji huyo baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu saba.

Baada y kuzungumza na kocha José Mourinho na kupata ruhusa ya Real Madrid, Essien anaamini kwamba njia bora zaidi ya kuwa 'fiti' tena ni kwenda kuwa chini ya uangalizi wa timu ya madaktari wa klabu yake ya London - jambo linalomaanisha kuwa kinachomsumbua ni muendelezo wa jeraha lake linalomsumbua kwa muda mrefu.

Essien ameichezea Real Madrid kwa miezi mitatu tu baada ya kujiunga nayo kwa mkopo. Kiungo huyo wa kimtaifa wa Ghana pia ameonekana akivaa tena jezi yake ya Chelsea yenye namba 5 mgongoni, ambayo klabu hiyo bado haijaitoa kwa mchezaji mwingine.

No comments:

Post a Comment