Friday, November 30, 2012

JB MPIANA JUKWAANI KUWASIKINDIKIZA MASHUJAA BAND LEADERS CLUB LEO

Rais wa bendi ya Wenge BCBG, JB Mpiana akizungumza baada ya kutua jijini Dar es Salaam
BENDI ya Mashujaa leo inazindua albamu yake ya pili ijulikanayo kwa jina la "Risasi Kidole" pamoja na bendi maarufu ya Congo, Wenge BCBG iliyochini ya mwanamuziki JB Mpiana kwenye  viwanja vya Leaders Club.

Uzinduzi huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa meneja wa bendi ya Mashujaa, Martin Sospeter.

Sospeter alisema kuwa wamejiandaa vilivyo katika uzinduzi huo na lengo lao kubwa ni kuweka historia katika muziki wa Tanzania.

Alisema kuwa wamekaa kambini muda wa siki mbili na wameandaa vitu vingi vipya kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki wa dansi nchini. Alisema kuwa kuna rap ya Ua Mbu na Dume la Simba kutoka kwa marapa wao, Saulo Ferguson na Sauti Radi.

Alifafanua kuwa wanamuziki wake wameadhimia ‘kufunika’ katika uzinduzi huo kwani anahistoria nzuri katika muziki wa Tanzania na kufanya kazi katika bendi nyingi.

“Tunawaomba Watanzania waje waone nini tunakifanya mbele ya gwiji la muziki wa dansi Afrika, JB Mpiana, najua wao wamepania, lakini sisi tumepania vilivyo kusafisha nyoyo za mashabiki ambazo kwa sku nyingi hawajapata burudisha la mioyo zao,” alisema.

Kiongozi wa bendi hiyo, Chaz Baba alisema kuwa wamepania kutoa somo kwa wanamuziki wa dansi hapa nchini ambao wamekuwa wakisubiri waone watafanya nini.

Alisema kuwa wameandaa nyimbo nyingi nzuri  na wamepatia kutawala soko la muziki hapa nchini.

“Njooni muone nini tunafanya katika muziki wa dansi, kambi yetu imekuwa nzuri na mafanikio makubwa, naomba mashabiki waje kutuunga mkono nasi tutawaunga mkono kwa kutoa burudani safi,”alisema Chaz.

Albamu ya Risasi Kidole ina jumla ya nyimbo sita. Nyimbo hizo ni Umeninyima, Tikisika, Hukumu ya Mnafiki, Ungenieleza, Kwa Mkweo na wimbo uliobebab jina la albamu hiyo, Risasi Kidole.

No comments:

Post a Comment