Tuesday, November 13, 2012

MARIO BALOTELLI ALIKOROGA TENA MANCHESTER CITY... SASA AJIWEKA KATIKA HATARI YA KUUZWA NA KURITHIWA NA FALCAO ATAKAYENUNULIWA KWA SH. BILIONI 112...!

Mario Balotelli
MANCHESTER, England
STRAIKA Mario Balotelli wa Manchester City anakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kuuzwa kufuatia vitendo vyake vya nje ya uwanja.

Gazeti la The Sun limesema kuwa mchezaji huyo yuko mbioni kuuzwa na Manchester City baada ya kuhudhuria sherehe za usiku kabla ya mechi yao ya Ligi Kuu ya England Jumapili iliyopita dhidi ya Tottenham ambayo walishinda 2-1.

Balotelli alionekana akiingia katika mgahawa na baa ya Panacea, eneo la Alderley Edge saa 7:00 usiku -- huku Man City wakicheza saa 7:30 mchana unaofuata dhidi ya Tottenham. Muitalia huyo (22), alitazama mechi hiyo akiwa jukwaani.

Hilo linamaanisha kuwa kocha Roberto Mancini sasa ataruhusiwa kumsajili mshambuliaji Radamel Falcao wa Atletico Madrid kwa ada itakayovunja rekodi ya klabu hiyo ya paundi za England milioni 45 (Sh. bilioni 112), mara tu baada ya kuachana na Balotelli. Tukio la sasa ndilo la karibuni zaidi kumhusisha Balotelli, kijana mtukutu wa Man City.

Shuhuda wa tukio hilo alisema: “Alifika Panacea akiwa na wapambe kibao na, nadhani hakuwa amevalia kwa ajili ya mtoko.

“Nilishangazwa kuona kwamba hakujali kuonekana akiwa kwenye pati muda mfupi kabla ya mechi, hata kama alijua kuwa hatacheza au hachezi.”
 

No comments:

Post a Comment