Tuesday, November 13, 2012

LIONEL MESSI ATUA SAUDI ARABIA NA KUZUA BALAA... MASHABIKI KIBAO WAFURIKA UWANJA WA NDEGE WAKITAKA NAFASI YA KUMUONA 'LIVE' NA WENGINE MAUJIKO YA KUMGUSA MKONO... ASKARI KIBAO WALAZIMIKA KUMLINDA NA BUNDUKI 'MAN TO MAN'

Tobaaa...! Mcheki Lionel anavyolindwa asikaribiwe na mashabiki huku akionekana kujawa na hofu kutokana na mtutu wa bunduki kuwa karibu na uso wake wakati alipotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme  Khaled jijini Riyadh, Saudi Arabia.



Pita huku...! Lionel Messi akielekezwa njia salama na mmoja wa maafisa wa Chama cha Soka cha Saudi Arabia.
Afu' tokea njia hii... Messi akiendelea kuonyeshwa njuia poa ya kupita kukwepa umati wa mashabiki waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Mfalme Khaled jijini Riyadh ili kumuona mshindi mara tatu mfululizo wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka wa Dunia.

Subiri kidogo tupate picha ya kumbukumbu...! Maafisa wa Saudia wakiacha kazi yao ya kumuelekeza Messi njia sahihi ya kupita na kuamua kupata picha ya ukumbusho.

Duh... sijui tupitie wapi kukwepa hawa wananchi! Afisa wa usalama wa Saudia akifikiria kupata upenyo mzuri wa kumtoa Messi ili kuwatoroka mashabiki kibao waliofika kwenye Uwanja wa Ndege wa Khaled jijini Riyadh kwa nia ya kumuona.

RIYADH, Saudi Arabia
Kulikuwa na vurugu zisizokuwa za kawaida kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme Khaled jijini Riyadh baada ya kuwasili kwa kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kujiandaa na mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Saudi Arabia kwenye Uwanja wa Mfalme Fahd kesho Jumatano.

Maafisa wa Uwaja wa Ndege walilalamikia kitendo cha maelfu ya mashabiki kufika uwanjani na kulazimisha wapewe nafasi ya kumuona nyota wa Argentina na klabu ya Barcelona ya Hispania, Lionel Messi.

Licha ya ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na silaha za moto kwenye uwanja wa ndege na pia katika barabara nzima ya kuelekea uwanjani, bado mamia ya mashabiki wa Messi walifanikiwa kupenya na kufika uwanjani.

Straika huyo alifika jijini Riyadh kwa ndege yake binafsi pamoja na familia yake kabla ya kuwasili kwa wachezaji wengine.

Hata hivyo, askari kibao waliokuwa uwanjani walitumia 'akili' za ziada kuwapiga chenga mashabiki na kufanikiwa kumuondoa Messi uwanjani.

Mashabiki wengi na maafisa wa usalama walilaumu vurugu za kulazimisha kumuona Messi kweny uwanja wa ndege, wakisema kwamba ishara hiyo si nzuri kwa timu ya taifa ya Saudi.

Waandishi wa habari pia walikuwa na kazi kubwa ya kuripoti tukio la ujio wa Messi na wenzake kwani walizuiwa kuwapo kwenye ukumbi ambao wachezaji walikusanyika.

No comments:

Post a Comment