Saturday, November 3, 2012

LIONEL MESSI APATA MTOTO WAKE WA KWANZA HATIMAYE... NI WA KIUME KAMA ILIVYOTARAJIWA NA MWENYEWE ACHEKELEA HUKU AKIMPATIA JINA LA THIAGO... AMEZAA NA DEMU WAKE YULE WA 'LONGTAIM KITAMBO' AITWAYE ANTONELLA ROCCUZZO

Mwanangu atatisha uwanjani kama mimi...! Messi akionyesha wa jezi maalum ya Barca kwa ajili ya mwanawe Thiago, mgongoni ikiwa na namba 10 ambayo ni ya kwake.
Twenzetu kliniki...! Hapa Messi akiwa na mzazi mwenzie, Antonella Rocuzzo kabla ya kuzaliwa kwa mtoto wao, Thiago Messi.
Hi...! Hapa Messi na mchumba wake Antonella wakiingia ukumbini kwenye sherehe za harusi ya mshkaji wao Andres Iniesta Julai 8, 2012.

Siku ya harusi ya Iniesta...Messi na mchumba wake Antonella wakiingia ukumbini. Hapa ni kabla ya kuzaliwa kwa Thiago.

Enzi hizoooo...! Messi akiwa ufukweni na mzazi mwenzie, Antonella Roccuzzo. Hapa hata ujauzito wa Thiago bado.

Messi na Mama Thiago, Antonella Roccuzzo... hapa penzi bado biiiichi! Ni longtaim kitambo!

Messi na Antonella walivyokuwa wakijiachia ufukweni kabla kupata mtoto
Nasi tutafanikiwa kweli kupata mtoto? Hapa Messi na 'girlfriend' wake Antonella walikuwa bado 'hawajatengeneza' ujauzito wa mtoto wao, Thiago Messi.

Hapa wote walikuwa bado 'serengeti ''....bila shaka hata wazo la kupata mtoto aitwaye Thiago lilikuwa halijagonga vichwani mwao.

Leo Messi amekuwa baba mapema leo (Ijumaa Novemba 2, 2012). Mtoto huyo wa kwanza wa Messi ambaye ni wa kiume aitwaye Thiago Messi, alizaliwa saa 11:15 jioni kwa saa za Hispania, kwenye Hospitali ya USP Dexeus mjini Barcelona.

Messi anayefahamika pia kwa jina la utani la 'La Pulga' hakufanya mazoezi na wenzake kwani katika mida ya kujifua yeye alikuwa kando ya mchumba wake kusubiria ujio wa mtoto wao wa kwanza. Messi ameahidi kuwa magoli atakayofunga baada ya tukio la leo atayatoa zawadi kwa mwanawe.

Muda mfupi tu baada ya kuzaliwa kwa mwanawe, straika huyo nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina alituma ujumbe ufuatao kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook: "Leo, nimekuwa mtu mwenye furaha zaidi ulimwenguni. Mwanangu amekuja duniani, asante Mungu! asante familia yangu kwa kuniunga mkono! Namtakia kheri kjila mmoja!".

Habari hizo zimetawala kwenye vyombo vya habari, hasa kwavile zilianza 'kubamba' tangu wiki iliyopita wakati iliporipotiwa kwamba Thiago Messi yuko mbioni kuzaliwa.

Wakati mashabiki wa Barça wakifurahia habari za kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza wa Messi, kocha Tito Vilanova amethibitisha kuwamo kwa straikia huyo kikosini katika mechi yao ya kesho (Jumamosi Novemba 3, 2012) dhidi ya Celta Vigo: "lakini ikiwa kila kitu kitakwenda sawa."

No comments:

Post a Comment