Friday, November 30, 2012

KWA WENZETU BWANA....! MTAZAME CRISTIANO RONALDO AKITOKA VIWANJA VYA USIKU NA DEMU WAKE IKIWA NI SIKU MBILI TU KABLA YA KUCHEZA MECHI KALI YA MAHASIMU WA JIJI KATI YAO REAL MADRID NA ATLETICO YA KINA RADAMEL FALCAO LEO JUMAMOSI DESEMBA 1


Ronaldo akiwa na mpenzi wake Irina Shayk (kushoto) na Izabel Goulart (katikati).

Ronaldo akitoka ukumbini akiwa beneti na mpenzi wake Irina Shayk pamoja na Izabel Goulart

Ronaldo akiwa na wanamitindo, mpenzi wake Irina Shayk pamoja na Izabel Goulart  

Mpenzi wa Ronaldo, mwanamitindo Irina Shayk.
Irina Shayk.
Tofauti na hapa Tanzania ambapo wachezaji kama wa Simba na Yanga hulazimika kuchungwa muda wote siku chache kabla ya mechi kali za ligi, kwa wenzetu hali ni tofauti sana.

Straika Cristiano Ronaldo wa klabu ya Real Madrid alionekana juzi usiku jijini Madrid akiwa katika tafrija ya kutambulisha toleo la Desemba la Vogue Spain huku akiwa na warembo wawili ambao ni wanamitindo -- Irina Shayk ambaye ni demu wake pamoja na Izabel Goulart.

Ronaldo alionekana akiwa 'beneti' na warembo hao ndani ya gari lake na walipotembea kwa miguu, mara zote alikuwa nao 'man to man', ikiwa ni siku mbili tu kabla ya mechi yao kali ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania watakayocheza leo Jumamosi (Desemba 1, 2012) dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Madrid, klabu ya Atletico Madrid inayoongozwa na straika wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao.

No comments:

Post a Comment