Friday, November 30, 2012

PLATINI: "KAMA MESSI ATASHINDA TUZO YA BALLON D'OR, NI KWA SABABU ANASTAHILI"

Messi (kushoto) akiwa na rais wa UEFA, Michel Platini

MFARANSA Michel Platini alitwaa tuzo ya Ballon d'Or mara tatu mfululizo (mwaka 1983, '84 na '85). Messi huenda akaipiku rekodi yake msimu huu. "Rekodi zipo ili zivunjwe. Kama atashinda tena, ni kwa sababua nastahili. Ana umri wa miaka 25 na ana kila fursa ya kuweka rekodi zake," alisema rais huyo wa UEFA katika mahojiano na jarida la 'France Football'.

Platini alitoa maoni yake kuhusu soka la Ufaransa na timu yake ya taifa. Katika maoni yake, Zidane anaweza kuwa kocha Ufaransa siku moja. "Mtu kama Zidane anaweza kuwa kocha. Wakati mwingine unazungumza naye na anasaidia kukuweka katika njia sahihi. Kutokana na uzoefu, najua si rahisi kuwa kocha bila ya kuifanya kazi hiyo kabla," alisema.

Hata hivyo, benchi la timu ya taifa ya Ufaransa kwa sasa linakaliwa na Didier Deschamps. "Alikuwa bonge la mchezaji na amekuwa na mafanikio katika kazi ya ukocha. Yeye ni mtu sahihi kabisa," alihakikisha Platini.

Messi pia alipata sapoti ya wachezaji wengi zaidi waliopendekeza ashinde tuzo ya Ballon d'Or. Jarida la 'France Football' liliuliza wanasoka 13 kutoa maoni yao. Saba kati yao walimchagua Muargentina huyo, watatu walimchagua Cristiano, mmoja aliwachagua Iniesta na Pirlo na wawili walikwepa kujibu. Waliomchagua Messi walikuwa ni Kopa, Luis Suarez, Keegan, Rummenigge, Van Basten, Sammer na Shevchenko. Rivera, Kaka na Beckenbauer walimchagua mshambuliaji Mreno wa Real Madrid, Ronaldo. Iniesta na Pirlo walipata kura kutoka kwa Cannavaro, wakati Di Stéfano na Figo waliamua "kukalia" maoni yao.

No comments:

Post a Comment