Wednesday, November 7, 2012

KWA MSAADA WA WANAWAKE, OBAMA ASHINDA URAIS MAREKANI KWA MARA YA PILI

Rais wa Marekani Barack Obama akishangilia na mkewe Michelle Obama na binti zao Malia (kulia) na Sasha baada ya ushindi wa uchaguzi mjini Chicago, leo Novemba 7, 2012. REUTERS
Wakenya wakishangilia kwenye viunga vya Kibera baada ya Barack Obama kutangazwa mshindi wa urais wa Marekani kwa mara ya pili
Wakenya wakishangilia kwenye viunga vya Kibera baada ya Barack Obama kutangazwa mshindi wa urais wa Marekani kwa mara ya pili

Wakenya wakishangilia kwenye viunga vya Kibera baada ya Barack Obama kutangazwa mshindi wa urais wa Marekani kwa mara ya pili

Mkenya katika kiunga cha Kibera akiweka 'kikombe' cha uji kwenye picha kubwa ya Obama katika kusherehekea Barack Obama kutangazwa mshindi wa urais wa Marekani kwa mara ya pili

Wakenya wakishangilia kwenye viunga vya Kibera baada ya Barack Obama kutangazwa mshindi wa urais wa Marekani kwa mara ya pili
Wanaomsapoti Obama wakisikiliza hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi
Obama akihutubia kushukuru baada ya kutangazwa mshindi
Rais wa Marekani Barack Obama akishangilia na mkewe Michelle Obama na binti zao Malia (kulia) na Sasha baada ya ushindi wa uchaguzi mjini Chicago, leo Novemba 7, 2012. REUTERS


Wamarekani wakishangilia baada ya Obama kushinda urais kwa kipindi cha pili 

TV ikionyesha habari za kuchaguliwa tena kwa Rais wa Marekani Barack Obama

Wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani, wageni wa Iraqi na mabalozi wakisikiliza hotuba ya rais aliyechaguliwa tena Barack Obama kwenye televisheni kwenye ubalozi wa Marekani mjini Baghdad leo Novemba 7, 2012. Picha: REUTERS

WASHINGTON, Marekani
KATIKA wiki ya mwisho ya kampeni za urais wa Marekani, tangazo moja lilitawala sana katika jimbo la Wisconsin. Liliwashirikisha wanawake watatu walioitwa Connie, Kim, na Anita ambao waliwaambia watazamaji sababu kwanini wamebadili msimamo yao kutoka kumsapoti Rais Barack Obama na kuhamia kwa Mitt Romney.

Kampeni za chama cha Republican zilitarajia kwamba wanawake kote Marekani wangefuata mwongozo wa wanawake hao watatu, lakini Obama aliweza kuwabakisha wapiga kura wake wa kike katika safari ya kuelekea kushinda uchaguzi huo jana Jumanne.

Obama alimshinda Romney kwa asilimia 55 dhidi ya 43 katika kura za wanawake, kwa mujibu wa takwimu za kura. Ushindi huo wa asilimia 12 unakaribia ushindi wa Obama wa tofauti ya asilimia 13 za wanawake alizopata dhidi ya mgombea wa Republican, John McCain mwaka 2008.

Romney hakufanya vyema kwa upande wa wanawake, ambao waliwashinda wapiga kura wanaume kwa asilimia 6, zaidi ya alivyofanya McCain miaka minne iliyopita.

Msingi mkubwa kwa mafaniko ya Obama: masuala ya kijamii. Takribani mara mbili ya wanawake wanaona masuala kama ya utoaji mbimba na ndoa za jinsia moja ndiyo mambo muhimu yanayoamua kura zao, kwa mujibu wa takwimu.

Kuanzia kongamano la Democrats, hotuba za Obama hadi matangazo ya kampeni, timu ya rais iliweka mbele mambo kama usawa na afya kwa wanawake vimekuwa ndio kitovu cha mijadala katika kuchaguliwa kwake tena.

Wamemponda Romney kwa kukosa msimamo kuhusu suala la utoaji mimba na haki za usawa tangu uchaguzi wa mwaka 2002 kama gavana wa Democratic na kushindwa kusapoti muswada wa Obama wa kurahisisha njia ya wanawake kuwashitaki waajiri wanaowafanyia unyanyasaji wa kimalipo.

Kwenye kituo cha kura cha Maplewood, New Jersey, Jumanne, mwanamama Rose Rios, 40, mwanachama wa Republican ambaye mara mbili alimpigia kura George W. Bush, alisema amepempia kura Obama kwa sababu anaona Romney ana misimamo mikali kuhusu jamii.

"Republicans hawawakilishi mitazamo ya ... wanawake wanaojitegemea," Rios alisema.

Wanawake wanaona masuala ya afya kama jambo lao kubwa linalowagusa, kwa mujibu wa takwimu za Reuters/Ipsos

No comments:

Post a Comment