Wednesday, November 14, 2012

KHEDIRA APONA NA KUJIFUA NA WENZAKE REAL MADRID... KARIM BENZEMA, MESUT OZIL, CRISTIANO RONALDO BADO WASUMBULIWA...WASHINDWA KUJIFUA NA WENZAO

Sami Khedira
MADRID, Hispania
KIUNGO Sami Khedira amepona jeraha la misuli ya paja na kurejea katika mazoezi ya kawaida na wachezaji wenzake wa kikosi cha kwanza cha Real Madrid tangu Jumapili waliposhinda 2-1 dhidi ya Levante.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani alijitonesha jeraha hilo wakati wa mechi yao ya kwanza ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund nchini Ujerumani.

Hata hivyo, mambo si mazuri sana kwa kocha Jose Mourinho wa Real Madrid kwani kuna wachezaji wengine kadhaa walioshindwa kujifua na wenzao kutokana na majeraha, wakiwamo mastraika Karim Benzema na Cristiano Ronaldo na pia kiungo-mshambuliaji Mesut Özil.

No comments:

Post a Comment