Wednesday, November 14, 2012

DAVID VILLA HAKUMPONGEZA MESSI KWA GOLI LA KWANZA


STRAIKA wa kimataifa wa Hispania, David Villa, ambaye ameripotiwa kuwa na bifu na straika mwenzake wa timu hiyo Lionel Messi, hakujumuika na wenzake kumpongeza Muargentina huyo wakati alipofunga goli la kwanza dhidi ya Real Mallorca.

Goli hilo lilikuwa ni la kihistoria kwani Messi alikuwa ameifikia rekodi ya Pele ya kufunga magoli 75 katika mwaka wa kalenda (kati ya Januari 1 - Desemba 31) iliyowekwa na gwiji huyo wa Brazil tangu mwaka 1958.

Na wakati Messi alipofunga goli lake la pili, Villa hakuwamo uwanjani kwani alishapumzishwa.

Tukio hilo linamwagia petroli moto wa uvumi kwamba wawili hao hawaivi chungu kimoja.

Iliripotiwa mapema kwamba Messi alimbwatukia Villa baada ya kumnyima pasi na kisha kupaisha mpira wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Granada na kisha, akamyima tena pasi na kupaisha mpira mjini Glasgow katika mechi dhidi ya Celtic.

No comments:

Post a Comment