Tuesday, November 20, 2012

JOSE MOURINHO KUANDIKA REKODI UEFA KESHO... ATAKUWA KOCHA MDOGO KULIKO WOTE KUWAHI KUONGOZA TIMU KATIKA MECHI 100 ZA LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA... NI WAKATI TIMU YAKE REAL MADRID ITAKAPOSHUKA ETIHAD KUCHEZA DHIDI YA MAN CITY...! ATAKUWA KOCHA WA TANO KATIKA HISTORIA KUFIKIA MECHI 100 AKILA SAHANI MOJA NA ALEX FERGUSON, ARSENE WENGER, CARLO ANCELOTTI, OTTMAR...!


MANCHESTER, England
Uongozi wake katika mechi ya Real Madrid dhidi ya Manchester City kesho Jumatano (Novemba 21, 2012) utamfanya José Mourinho awe kocha mwenye umri mdogo kuliko wote kuwahi kufikia rekodi ya mechi 100 za Ligvi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Mourinho pia atakuwa kocha wa tano katika historia kufikia idadi hiyo ya mechi, akiungana na magwiji wengine wanne ambao ni Carlo Ancelotti, Arsène Wenger, Ottmar Hitzfeld na Alex Ferguson.

Mourinho atafikia rekodi hiyo akiwa na miaka 49 tu, hivyo kuandika rekodi ya kuwa kocha mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya michuano hiyo ya juu kwa ngazi ya klabu barani Ulaya .

Aliyewahi kushikilia rekodi ya kufikia idadi ya mechi 100 akiwa mdogo zaidi hapo kabla alikuwa Carlo Ancelotti, aliyekuwa na miaka 51. Wenger na Hitzfeld walifikia mechi 100 wakiwa na miaka 58, wakati Ferguson alikuwa na 62.

Kocha huyo Mreno, aliyewahi kuziongoza klabu nne (Porto, Chelsea, Inter na sasa Real Madrid) katika michuano hiyo, ataweka rekodi mpya kwa kuwa mdogo kwa miaka miwili zaidi.

Cha kufurahisha, ilikuwa ni kwenye Uwanja wa Bernabéu ambako Mou, atakayekuwa akiiongoza Real katika mechi yake ya 29 ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tangu atue Real Madrid baada ya filimbi ya mwisho kesho, alikoanza kuongoza timu katika michuano hiyo FGebruari 19, 2002. Tangu wakati huo, rekodi yake inasomeka: Ushindi mechi 54, sare 25 na vipigo 20, huku timu zake zikifunga magoli 166 na kufungwa 85.

Takwimu zinazungumza, kwamba 'Special One' alikuwa na matokeo mazuri zaidi msimu uliopita, wakati timu yake ya Real Madrid ilipofungwa na Bayern katika nusu fainali. Licha ya kushindwa kutwaa taji, timu yake iliweka rekodi kwa kupata matokeo bora zaidi kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kushinda mechi 10 kwa ujumla, wakipata sare na kufungwa katika mechi moja tu na kufunga magoli 35 (wastani wa magoli matatu katika kila mechi).

No comments:

Post a Comment