Tuesday, November 20, 2012

ATHUMANI NYAMLANI WA TFF APEWA SHAVU FAINALI AFCON 2013... NI BAADA YA KUTEULIWA KUWA MJUMBE KAMATI YA RUFANI YA MICHUANO HIYO AFRIKA KUSINI!

Athumani Nyamlani
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani amepata 'shavu' nene baada ya kuteuliwa na Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Issa Hayatou kuwa mmoja wa wajumbe watatu wa kamati ya rifani ya fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2013) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, amesema leo (Novemba 20) kuwa Nyamlani atashirikiana na Mcameroon Prosper Abega na afisa mwingine kutoka Gabon kuongoza kamati ya rufaa kwenye fainali hizo zitakazoanza Januari 19, 2013.

Nyamlani pia ni mjumbe wa Bodi ya Rufani ya CAF yenye wajumbe 12 na wajumbe watatu walioteuliwa ni miongoni mwa wajumbe hao.

No comments:

Post a Comment