Tuesday, November 6, 2012

IKER CASILLAS AMSHANGAA CRISTIANO RONALDO KWA KUSEMA ATAJICHAGUA MWENYEWE KATIKA UPIGAJI KURA KUMPATA MWANASOKA BORA WA DUNIA ‘FIFA BALLON D'OR’


Hureeeeee...! Kipa Iker Casillas (kushoto) na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid wakishangilia wakati wakipita na gari la wazi mitaa ya Plaza de Cibeles jijini Madrid, Mei 3, 2012, baada ya kutwaa kwa mara ya kwanza ubingwa wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania walioukosa tangu mwaka 2008. Ubingwa huo pia ulikuwa wa 32 katika historia yao.  
MADRID, Hispania
Nahodha wa Real Madrid, Iker Casillas amekaribisha tena mjadala kuhusu mahusiano yake na mchezaji mwenzie, Cristiano Ronaldo baada ya kutoa maoni ya kumponda mshambuliaji huyo kuhusiana na Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia (FIFA Ballon d'Or 2012).

Mwishoni mwa wiki, Ronaldo alisema kuwa atajipigia kura yeye mwenyewe, huku akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kujiweka nyuma.

Lakini Casillas, amesema: "Kwakweli, mimi siwezi (kujipigia mwenyewe). Ningependa sifa zitokanazo na kazi yangu zitoke kwa watu wengine, badala ya mimi mwenyewe."

Kipa huyo aliendelea kueleza kwamba atamtanguliza Sergio Ramos kabla ya Ronaldo katika kumchagua mshindi wa tuzo ya FIFA Ballon d'Or.

No comments:

Post a Comment