Thursday, November 15, 2012

ZLATAN IBRAHIMOVIC AITESA ENGLAND KWA KUWAPIGA GOLI NNE LIKIWAMO KALI LA 'BAISKELI' KUIPA SWEDEN USHINDI WA 4-2 ... MSITU WA MABEKI SAUDI ARABIA WAMFUNIKA LIONEL MESSI WAKATI ARGENTINA IKISHIKILIWA KWA SARE YA 0-0... LUIS SUAREZ AIPA RAHA URUGUAY, NEYMAR AIOKOA BRAZIL ISIADHIRIWE NA COLOMBIA YA KINA FALCAO... UFARANSA YAITANDIKA ITALIA 2-1.. DIDIER DROGBA AENDELEZA MOTO WAKE NA KUIPA IVORY COAST USHINDI 3-0 DHIDI YA AUSTRIA...!

Straika wa Ivory Coast, Didier Drogba akiwaacha watu wakati wa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Austria mjini Linz jana Novemba 14, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Ivory Coast, Lacina Traore (kushoto) wa klabu ya Anzhi Makhachkala, akifunga goli huku beki wa Austria, Sebastian Proedl akijaribu kumzuia wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa mjini Linz jana Novemba 14, 2012. Picha: REUTERS
Zlatan Ibrahimovic (kushoto) wa Sweden akishangilia huku Danny Welbeck wa England akirejea kiunyonge baada ya Zlatan kufunga goli lake la nne jana. Sweden ilishinda 4-2.
Hivi ndivyo alivyojipinda kupiga goli kali la nne....! Straika Zlatan Ibrahimovic wa Sweden akiruka hewani na kupiga shuti la 'baiskeli'  kufunga goli la kusisimua la nne nne dhidi ya England wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kwenye Uwanja wa 'Friends Arena' mjini Stockholm, Sweden jana usiku Novemba 14, 2012. (Picha: AP)



Zlatan Ibrahimovic wa Sweden akishangilia baada ya kufunga goli lake la kwanza dhidi ya England wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kwenye Uwanja wa 'Friends Arena' mjini Stockholm, Sweden jana usiku Novemba 14, 2012. (Picha: AP)

Hapa leo hupati kitu...straika Lionel Messi wa Argentina (kulia) akijaribu kupita 'msitu' wa mabeki wa Saudi Arabia waliokuwa wakimchunga muda wote wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kwenye Uwanja wa Mfalme Fahd jijini Riyadh, Saudi Arabia jana Novemba 14, 2012. Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 0-0. (Picha: AP)

Straika Lionel Messi wa Argentina akijaribu lkuwatoka mabeki wa Saudi Arabia wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kwenye Uwanja wa Mfalme Fahd jijini Riyadh, Saudi Arabia jana Novemba 14, 2012. Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 0-0. (Picha: AP)

We nuksi hatukuachio ng'o... Mabeki wa Saudi Arabia (kushoto) wakimfukuza kwa kasi straika Lionel Messi wa Argentina wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kwenye Uwanja wa Mfalme Fahd jijini Riyadh, Saudi Arabia jana Novemba 14, 2012. Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 0-0. (Picha: AP)

Huendi kokote....! Sergio Aguero wa Argentina (kushoto) akibanwa na Moataz Al-Musa wa Saudi Arabia wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kwenye Uwanja wa Mfalme Fahd jijini Riyadh, Saudi Arabia jana Novemba 14, 2012. Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 0-0. (Picha: AP)

Straika Didier Drogba wa Ivory Coast (kushoto) akishangilia goli alilofunga dhidi ya Austria wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki mjini Linz, Austria jana usiku Novemba 14, 2012.

Safiiiii.....! Straika Didier Drogba (kushoto) wa Ivory Coast akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli la pili dhidi ya Austria wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki mjini L;inz, Austria jana usiku Novemba 14, 2012.

Drogba (kushoto) wa Ivory Coast akishangilia na  Kolo Toure (katikati) baada ya kufunga goli dhidi ya Austria wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki mjini L;inz, Austria jana usiku Novemba 14, 2012.
Tunatisha...! Kiungo mkabaji Tcheik Tiote wa Ivory Coast akishangiolia goli mojawapo walilofunga dhidi ya Austria wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki mjini Linz, Austria  jana usiku Novemba 14, 2012.!

Mario Alberto Yepes wa Colombia (kulia) akimvuta straika Neymar wa Brazil wakati wa mechi yao ya kimtaifa ya kirafiki kwenye Uwanja wa MetLife jana Novemba 14, 2012. Zilitoka sare ya 1-1 (Picha: AP)

Hivi sasa ndo' nini ...! Straika Neymar wa Brazil akilalamika baada ya kuangushwa na beki Mario Alberto Yepes wa Colombia wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Colombia jana usiku Novemba 14, 2012.

Gooooohhhh....! Straika Bafetimbi Gomis wa Ufaransa (kushoto) aklishangilia goli la ushindi alilofunga dhidi ya Italia wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Italia jana usiku Novemba 14, 2012.


Kipa wa England, Joe Hart akiokoa hatari langoni mwake.... zingekuwa nyingi!!!

Kipa wa England, Joe Hart akiokoa hatari langoni mwake.... zingekuwa nyingi!!!

Straika wa England, Wilfried Zaha akiwa benchi pamoja na Jack Wilshere kabla ya kuingia katika mechi yao dhidi ya Sweden.




Straika wa Italia, Mario Balotelli (kulia) akimpongeza El Sharaawy kwa kufunga goli dhidi ya Ufaransa....

Straika wa Ubelgiji, Lukaku akijilaumu kukosa goli....

Straika wa Ubelgiji, Lukaku akijilaumu kukosa goli....

Wilfried Zaha wa England akijaribu kumuacha mtu..
.

El Sharaawy wa timu ya taifa ya Italia akishangilia bao lake dhidi ya Ufaransa. Italia walilala 2-1

Raheem Sterling akitafuta mbinu za kumpita mtu....

Kikosi cha timu ya taifa ya England kabla ya mechi yao dhidi ya Sweden

Kocha wa Zambia, Herve Reinard akiiongoza timu yake dhidi ya Bafana Bafana ya Afrika Kusini.





Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps akimpongeza Bafetimbi Gomes baada ya straika huyo kuifungia goli Ufaransa dhidi ya Italia





Straika wa England, Wilfried Zaha (kushoto) akijaribu kumuacha mtu...

Straika wa England, Wilfried Zaha

Straika wa England, Wilfried Zaha


Ibra wewe hufaiiii..... Steven Gerrard akimpongeza Zlatan Ibrahimovic. Wiki hii Zlatan alimshauri Gerrard atafute klabu nyingine inayoweza kutwaa mataji kabla umri haujamtupa mkono.

Straika wa England, Wilfried Zaha



Straika wa England, Wilfried Zaha







Kaka naomba jezi yako, ila nami wasinisimange kama Santos wa Arsenal.... Straika wa England, Danny Welbeck (katikati) akiomba jezi ya Zlatan Ibtrahimovic wa Sweden (kulia) huku Wilfried Zaha wa England akishuhudia baada ya mechi yao. Zlatan aliwapiga zote nne.

Beki wa Hispania, Sergio Ramos akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Panama






Straika wa Sweden akifunga kwa 'fri-kiki' dhidi ya England...

ZLATAN Ibrahimovic alifunga magoli MANNE, likiwamo la 'tiktaka' ya ajabu - wakati Sweden iliposherehekea uzinduzi wa uwanja wao mpya kwa ushindi wa 4-2 dhidi ya Egland.

Straika huyo wa klabu ya PSG aliwafungia Sweden goli la kuongoza kabla ya Danny Welbeck kuwasawazishia England.

Steven Caulker, mmoja wa wachezaji sita wa England ambao walikuwa wakiichezea timu hiyo ya taifa kwa mara ya kwanza, aliifungia timu yake goli la kuongoza lakini Ibrahimovic akasawazisha baada ya kumiliki kiufundi kifuani pasi ndefu kutoka nyuma na kuisawazishia Sweden.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 31 akafunga kwa 'fri-kiki' kali ya chini kabla ya kukamilisha ushindi kwa "goli la mwaka" kwa 'tiktaka' ya ajabu kutokea umbali wa yadi 30 baada ya kipa wa England Joe Hart kutoka nje ya boksi na kujaribu kuokoa mpira kwa kichwa kabla haujapaa jirani na Zlatan ambaye aliufuata huko huko juu akiwa amelipa mgongo goli na kubinuka 'tiktaka' atakayoikumbuka maishani iliyokwenda moja kwa moja wavuni.

Lilikuwa ni goli kali lililowafanya hata mashabiki wa England wampigie makofi straika huyo mwenye mwili mkubwa, ambaye alivua shati na kuruka hewani wakati akishangilia bao hilo la kipekee. 


DROGBA AING'ARISHA IVORY COAST, KINA MESSI HOI

Nahodha Didier Drogba aliendeleza moto wake wa kupachika mabao wakati alipokuwa  miongoni mwa wafungaji wakati timu ya taif ya Ivory Coast inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2013) ilipoibuka na ushindi mnono wa ugenini wa mabao 3-0 katika mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya  Austria usiku wa kuamkia leo.

Mkongwe Drogba, aliyehamia katika klabu ya Shanghai Shenhua inayoshiriki Ligi Kuu ya China mwaka jana baada ya kuisaidia Chelsea kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, alifunga katika dakika ya 61 mjini Linz kuipa Ivory Coast uongozi wa mabao 2-0.

Lacina Traore aliihakikishia Ivory Coast ushindi mnono wa 3-0 kwa taifa hilo linaloshikilia Na. 1 kwa viwango vya ubora wa soka barani Afrika wakati zikiwa zi9mesalia dakika 14 za muda wa kawaida wa mechi kumalizika baada ya Didier Ya Konan kuwafungia bao la utangulizi katika dakika ya 44.

Hayo yalikuwa ni matokeo mazuri kwa Ivory Coast, waliomkosa straika wa Arsenal anayesumbuliwa na jeraha, Gervinho, wakati wakijiandaa kabla ya kuwania ubingwa wa pili wa AFCON nchini Afrika Kusini mwakani.

Lionel Messi alichungwa muda wote na rundo la mabeki katika muda mwingi wa mechi na hivyo kushindwa kufurukuta kabisa wakati timu ya taifa lake ya Argentina ikishikiliwa kwa sare isiyotarajiwa ya 0-0 dhidi ya Saudi Arabia, wakati Ureno iliyomkosa nyota wao aliye majeruhi, Cristiano Ronaldo, pia ilishikiliwa kwa sare iya kushangaza ya 2-2 dhidi ya wenyeji Gabon. Pedro Rodriguez alifunga mabao mawili kuisaidia Hispania 'kuwakandamiza' wenyeji Panama mabao 5-1.

Katika Uwanja wa East Rutherford, Neymar alifunga katika dakika ya 64 na baadaye akapaisha penati waliyopata katika dakika ya 81, hivyo kuiacha Brazil ikipata sare isiyostahili ya 1-1 katika mechi waliyotawala kwa muda mwingi dhidi ya Colombia ambao walitangulia kufunga katika dakika ya 44 kupitia kwa Juan Guillermo Cuadrado.

Kwenye Uwanja wa Marlins Park mjini Miami, Ideye Brown na Igiebor Nosa walifunga ndani ya dakika 5 mwanzoni mwa kipindi cha pili kuipa Nigeria ushindi wa 3-1 dhidi ya Venezuela 3-1 katika mechi yao ya maonyesho. Edinson Cavani na Luis Suarez walikuwa ni miongoni mwa wafungaji walioipa Uruguay ushindi wa ugenini wa mabao 3-1 dhidi ya Poland.

Alikuwa ni Zlatan Ibrahimovic aliyetawala matokeo ya mechi za jana hata hivyo kutokana na bao lake la kusisimua la shuti kali la baiskeli, ambalo linaelezewa na nahodha wa England,  Steven Gerrard - aliyecheza mechi yake ya 100 ya kimataifa - kuwa  "ni miongoni mwa magoli bora niliyopata kuyaona moja kwa moja kwa macho yangu.''

''Wakati nilipoona kipa hayupo, nikajaribu kupiga shuti golini, na kwa bahati mpira ukaenda wavuni,'' amesema Ibrahimovic.

''Ni mchanganyiko wa bahati na ujuzi," aliongeza Ibrahimovic.

MATOKEO YA MECHI ZA KIRAFIKI ZILIZOCHEZWA USIKU WA KUAMKIA LEO

Panama 1-5 Hispania
Italia 1-2 Ufaransa
Poland 1-3 Uruguay
Jamhuri ya Ireland 0-1 Ugiriki
Austria 0-3 Ivory Coast
Gabon 2-2 Ureno
Hungary 0-2 Norway
Uholanzi 0-0 Ujerumani
Sweden 4-2 England
Luxembourg 1-2 Scotland
Chile 1-3 Serbia
Romania 2-1 Ubelgiji
Uturuki 1-1 Denmark
Israel 1-2 Belarus
Andorra 0-2 Iceland
Liechtenstein 0-1 Malta
Cyprus 0-3 Finland
Saudi Arabia 0-0 Argentina
Jamhuri ya Czech 3-0 Slovakia
Bulgaria 0-1 Ukraine
Armenia 4-2 Lithuania
Urusi 2-2 USA
China PR 1-1 New Zealand
Korea Kusini 1-2 Australia

No comments:

Post a Comment