Wednesday, November 21, 2012

DIDIER DROGBA AIOMBA FIFA IMSAIDIE KUIHAMA TIMU YAKE CHINA KWA MKOPO, AHUSISHWA NA CHELSEA, JUVENTUS

Didier Drogba akijifua na 'chama' lake la Shanghai Shenhua nchini China.
SHANGHAI, CHina
Straika wa Shanghai Shenhua, Didier Drogba ameiomba FIFA imsaidie kupata ruhusa ya kuhama kwa mkopo kutoka katika klabu yake ya sasa ili apate wasaa wa kujiweka 'fiti' kabla ya kuanza kwa fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika kuanzia Januari nchini Afriak Kusini.

Ligi Kuu ya China inamalizika mapema mwezi huu, na Drogba anajiandaa kuhama kwa muda kutoka Shenhua ili aendelee kulinda kiwango chake hadi fainali za AFCON zitakapoanza Januari 19, 2013, huku FIFA ikifikiria ombi la straika huyo nyota wa zamani wa Chelsea.

"Idara ya Utawala ya FIFA inaangalia namna ya kumsaidia,'' FIFA imesema katika taarifa yake.

Hivi karibuni, Drogba ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast, amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kwenda katika klabu mbalimbali kubwa zikiwamo za Juventus na Chelsea, lakini hatakuwa tayari kusajiliwa kabla ya Januari 1 kwa mujibu wa sheria za sasa za FIFA.

Ivory Coast imepangwa kundi moja na timu za taifa za Tunisia, Algeria na Togo katika Kundi D la fainali za AFCON 2013 . Itacheza dhidi ya Togo Januari 22 katika mechi yao ya kwanza kwenye michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment