Wednesday, November 21, 2012

RAFA BENITEZ AKIRI KUFUKUZIA NAFASI ILIYOACHWA NA DIMATTEO CHELSEA

Rafael Benitez
LONDON, England
KOCHA wa zamani wa Liverpool, Rafael Benitez amethibitisha kwamba ni kweli anafukuzia nafasi ya ukocha iliyoachwa wazi katika klabu ya Chelsea kufuatia kutimuliwa jana kwa kocha Roberto Di Matteo.

Mhispania huyo mwenye miaka 52 aliwahi kutwaa mara mbili taji la Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Liverpool mwaka 2005 na pia kumaliza katika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya England mwaka 2008-09, lakini akaondoka kwa makubaliano ya pande zote mwaka 2010.

"Ndiyo kwanza nimesikia (kuhusu Di Matteo). Ni wazi kwamba Chelsea ni klabu kubwa na inaweza kupigania mataji," amesema.

"Katika soka watu wanasema mengi kwa hiyo tutaona katika siku chache zijazo. Natafuta klabu inayoweza kupigania mataji na Chelsea ni miongoni mwa klabu hizo," ameongeza.

No comments:

Post a Comment