Thursday, November 22, 2012

BAO LA KARIM BENZEMA LAING'OA MANCHESTER CITY KLABU BINGWA ULAYA BAADA YA SARE YA 1-1... JACK WILSHERE, LUKAS PODOLSKI WATUPIA NA KUIPELEKA ARSENAL HATUA YA 16-BORA

Dah... ndo basi tena! Kutoka kushoto ni Yaya Toure, Vincent Kompany, Samir Nasri wa Man City wakionekana wapole baada ya kuifungwa goli la utangulizi na Karim Benzema wa Real Madrid katika mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Etihad, Manchester leo Novemba 21, 2012.
Goooooohhh....! Straika Karim Benzema wa Real Madrid akimfunga kipa Joe Hart wa Man City wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Etihad, Manchester leo Novemba 21, 2012.  
Lucas Podolski akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Montpellier wakati wa mechi yao ya Kundi B la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates, London leo Novemba 21, 2012.  

Jack Wilshere wa Arsenal (kulia) akifunga goli la  Arsenal dhidi ya Montpellier wakati wa mechi yao ya Ligi ya Kalbu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, leo Novemba 21, 2012.
MANCHESTER, England
Manchester City wameshindwa kufuzu kwa hatua ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya  kwa msimu wa pili mfululizo kufuatia sare ya nyumbani ya 1-1 waliyoipata usiku huu (Novemba 21, 2012) dhidi ya Real Madrid.

Man City walitakiwa kushinda lakini walijikuta wakipelekeshwa mwanzoni mwa mechi na kuruhusu goli la mapema wakati Karim Benzema alipotumia vyema krosi ya Angel Di Maria na kuukwamisha mpira wavuni kuipa Real bao la utangulizi.

Straika Sergio Aguero aliisawazishia Man City kwa penati baada ya mapumziko kufuatia faulo aliyochezewa na Alvaro Arbeloa ambaye alitolewa nje ya uwanja kwa kadi ya pili ya njano kutokakana na kosa hilo.

Real Aguero alikaribia kuipa Man City bao la pili katikati ya kipindi cha pili lakini kipa Iker Casillas akaokoa juu ya mstari wa goli.

Mbali na goli la Benzema, Real pia walipoteza nafasi kadhaa za wazi kuibuka na ushindi mnono, zikiwamo mbili zilizopotezwa na Khedira aliyekuwa amebaki na kipa na nyingine ya Ronaldo aliyobaki pia na kipa lakini shuti lake la mpira wa kubetua likaokolewa juu ya mstari na straika huyo akabaniwa tena wakati alipouwa mpira uliorudi na kupiga shuti lililomparaza Vincent Kompany na kuwa kona.

Matokeo hayo yaliihakikishia Real Madrid nafasi ya kufuzu kwa hatua ya 16-Bora pamoja na Borussia Dortmund, ambao waliishindilia Ajax mabao 4-1 na kubaki kileleni mwa msimamo wa kundi lao la D huku kila timu ikiwa imebakiza mechi moja --  Dortmund wakibakiwa na mechi ya nyumbani dhidi ya Man City na Real Madrid wakimalizia nyumbani pia kwa kucheza dhidi ya Ajax.

Katika mechi nyingine za leo, Arsenal ilijihakikishia nafasi ya kufuzu kwa hatua ya 16-Bora pia kutoka katika kundi lao la B baada ya magoli ya Jack Wilshere  na
Lukas Podolski kuwapa ushindi 'mtamu' wa nyumbani wa 2-0 dhidi ya Montpellier.

MATOKEO MECHI ZA UEFA LEO J'TANO NOV. 21
    Arsenal             2 - 0 Montpellier
    Man City          1 - 1 Real Madrid
    Zenit                 2 - 2 Malaga
    Ajax                 1 - 4 Dortmund
    Anderlecht       1 - 3 AC Milan
    Dynamo Kiev   0 - 2 PSG
    Porto                3 - 0 Zagreb
    Schalke            1 - 0 Olympiakos

No comments:

Post a Comment