Sunday, November 4, 2012

CRISTIANO RONALDO: "LIONEL MESSI NI MCHEZAJI MKALI... MIE KUCHEZA NAYE INAWEZEKANA LAKINI LABDA AJE HAPA (REAL MADRID)... ILA MIE KWENDA BARCAELONA NI JAMBO GUMU SANA"

Ronaldo na Messi
Katika mahojiano yake maalum na chaneli ya michezo ya televisheni ya Marekani iitwayo 'beIn Sport', Cristiano Ronaldo amesema kwamba hatakuwa na tatizo lolote kucheza pamoja na Lionel Messi.

"Kucheza na Messi? Kwanini isiwezekane? Hakuna tatizo – akija hapa (Real Madrid) tutacheza pamoja, lakini mimi kwenda kule (Barcelona) ni jambo gumu sana", amesema.

Cristiano pia alizungumzia tabia ya vyombo vya habari kupenda kumlinganisha yeye na Messi.

"Hilo jambo halijaanza sasa, ni tangu miaka mitano iliyopita – siku zote huwa hivyo. Siwezi kubadili jambo hilo. Sifanyi kazi kwenye magazeti, sifanyi kazi kwenye televisheni. Wanapenda kutulinganisha", alisema.

"Nini nitakachofanya? Napaswa kufanya kazi yangu, napaswa kujifua, napaswa kufunga magoli, napaswa kucheza, wakati wote napaswa kujaribu kuisaidia timu yangu na sio kufikiria jambo hilo", ameongeza.

CR7 amekiri kwamba mchawi huyo wa Argentina yuko juu, lakini akaongeza kuwa uhusiano wao huishia ndani ya uwanja na si zaidi ya hapo.

"Messi ni mchezaji mkali. (Tuna) mahusiano ya kiuchezaji kama nilivyo na wachezaji wengine, siyo rafiki yangu kwa sababu hatushirikiani chumba cha aina moja cha kubadilishia nguo na hatutoki pamoja kwenda kupata mlo wa jioni, lakini namheshimu kama mchezaji wa kulipwa", amesema.

No comments:

Post a Comment