Sunday, November 4, 2012

BRIGITTE NDIYE MREMBO ZAIDI REDDS MISS TANZANIA 2012

Redds Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred (18) akipunga mkono baada ya kutangazwa mshindi wa taji hilo.
Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati) akipunga mkono baada ya kutangazwa mshindi wa taji hilo akiwa na mshindi wa pili, Eugene Fabian (kushoto) na mshindi wa tatu, Edda Sylvester. Brigitte anatokea Kitongoji cha Sinza Kanda ya Kinondoni wakati Eugene anatoka Mkoa wa Mara (Kanda ya Ziwa) huku Edda ni Miss Kigamboni (Kanda ya Temeke).
Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati)akionyesha funguo ya gari aina ya Toyyota Noah alilopewa kwa kushinda taji hilo la urembo nchini. Kulia ni Hashim Lundenga, mkurugenzi wa Lino Agency inayoandaa shindano hilo.

Wewe unastahili... Miss Tanzania wa mwaka jana Salha Israel (kushoto) akipozi kwa picha na Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred
Majaji wakiwa mzigoni

Mshiriki Anande Raphael akijipa stejini

Hamna maswali..... Brigitte Alfred akipita stejini kabla ya kutangazwa mshindi wa Redds Miss Tanzania 2012

Elizabeth Diamond akipita stejini

Happiness Rweyemamu akipita stejini

Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2012 wakiwa stejini kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam

MREMBO Brigitte Alfred (18) kutoka Kanda ya Kinondoni usiku wa jana alitwaa taji la urembo la taifa mwaka huu 'Redd's Miss Tanzania 2012' baada ya kuwashinda wenzake 29 katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Brigitte mwenye sura yenye mvuto, alionekana kukosa mpinzani tangu mapema na alifunika zaidi wakati alipojibu kiufasaha swali lake.

Kwa ushindi huo, Brigitte aliyeibukia katika shindano la Miss Sinza, alikabidhiwa funguo za gari jipya aina ya Toyota Noah na pia atapata fedha Sh. milioni nane.

Kimwana huyo pia ataiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia yatakayofanyika mwakani nchini Indonesia.

Baada ya kutangazwa mshindi, Brigitte alisema ametimiza ndoto zake.

"Nimefurahi sana na nawashukuru wote walionisaidia hadi nimefika hapa, naahidi kuliwakilisha vyema taifa langu katika shindano la Miss World mwakani," alisema.

Eugine Fabian (21) aliibuka mshindi wa pili na kujishindia zawadi ya Sh. milioni 6.2 na mrembo wa Kigamboni na mshindi wa taji la Kanda ya Temeke, Edda Sylivester (21) alishinda nafasi ya tatu na zawadi ya Sh. milioni nne.

Magdalena Roy aliibuka wa nne na zawadi ya Sh. milioni tatu wakati Happiness Daniel alikamilisha nafasi ya tano na kujishindia zawadi ya Sh. milioni 2.4 katika shindano hilo lililopamba na burudani kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz, Recho wa THT na msanii wa kiasili, Wanne Star.

Warembo wengine walioingia hatua ya 15 bora katika shindano hilo ni Lucy Stephano ambaye anashikilia taji ya Miss Photogenic, Babylove Kalala (Miss Talent), Mary Chizi (Miss Sports), Warid Frank, Happiness Rweyemamu, Phina Revocatus, Irene Veda, Joyce Baluhi na Catherine Masumbigana. Kila aliyeingia katika hatua hiyo atazawadiwa Sh. milioni 1.2.

Washiriki wengine 15 waliosalia ni pamoja na Zuwena Nassib, Lightness Michael, Vency Edward, Flaviana Maeda, Carren Elias, Fatuma Ramadhani, Belinda, Mbogo, Amanda Raphael, Jesca Haule, Naomi Jones, Diana Hussein, Kudra Lupato, Noela Michael, Rose Lucas, Virginia Mokiri na Elizabeth Diamond.

Warembo hao watakabidhiwa hundi zao usiku wa leo katika sherehe iliyoandaliwa na kesho watarejea makwao.No comments:

Post a Comment