Wednesday, November 21, 2012

ARSENE WENGER ASEMA ATAMSAJILI TENA THIERY HENRY MWEZI JANURI ILI AICHEZEE KLABU HIYO KWA MARA YA TATU... NIA NI KUZIBA PENGO LA SAFU YA MASTRAIKA LITAKALOACHWA NA GERVINHO NA CHAMAKH WATAKAOKWENDA 'SAUZI' KUSHIRIKI FAINALI AFCON 2013


Thierry Henry akishangilia bao aliloifungia Arsenal dhidi ya Leeds United wakati wa mechi yao ya raundi ya tatu ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Emirates jijini London Januari 9, 2012.
LONDON, England
Straika wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry anaweza kurudi tena kwenye klabu hiyo ya jiji la London kuichezea kwa mkopo wa muda mfupi akitokea katika klabu yake ya New York Red Bulls mwezi Januari, kwa mujibu wa kocha Arsene Wenger.

"Amekuwa akifanya mazoezi na sisi," Wenger amesema leo (Jumanne Novemba 21, 2012) kupitia tovuti ya klabu yao (www.arsenal.com).
"Nitamsajili tena Januari? Sijui. Siwezi kukataa. Ni mwepesi."

Straika huyo anayeshikilia rekodi ya kupachika mabao katika klabu ya Arsenal baada ya kufikisha magoli 228, sasa akiwa na miaka 35, alirejea katika klabu yake hiyo ya zamani Januari iliyopita, akafunga dhidi ya Leeds United katika mechi yao ya Kombe la FA na pia akawapa ushindi kwa goli pekee alilofunga kuelekea mwishoni mwa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Sunderland.

Wenger alifurahishwa na mchango wa Henry na anaamini kwamba anaweza kuwa mchezaji mughimu kwao kama atarejea tena kwa mara ya tatu, hasa ikiwa klabu yao itamkosa straika Gervinho wa Ivory Coast na straika wa Morocco,  Marouane Chamakh ambao watakwenda kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

"Mwaka jana nilimsajili kwa sababu tulimpoteza Gervinho. Ulikuwa ni muunganiko mzuri. Mwaka huu tutamkosa tena Gervinho kwavile watashiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka wa pili," alisema Wenger ambaye timu yake ilianza msimu huu kwa kusuasua.

"Kwa hiyo tutakabiliwa na upungufu. Hasa ikiwa Chamakh naye atakwenda kwenye fainali hizo. Siwezi kumzuia. Hapo tutakuwa na upungufu," ameongeza kocha huyo Mfaransa wakati akizungumza kabla ya mechi yao ya leo usiku katika Kundi B la Ligi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Montpellier.

Wenger anajua kuwa Henry, ambaye ametoka kumaliza msimu wa Ligi Kuu ya Marekani baada ya klabu yake ya Red Bulls kufungwa na D.C United katika nusu fainali ya ligi hiyo ukanda wa Mashariki, ni mchezaji mwenye ushawishi mkubwa kikosini awapo ndani na nje ya uwanja.

"Unajua nini anachokupa. Anakupa matumaini, hasa anapoingia uwanjani. Hicho nd'o kitu muhimu zaidi," amesema.

"Yeye ni mzungumzaji. Mcheshi. Ana akili sana. Anaweza kutoa ushauri mzuri kwa wachezaji kwa sababu alikuwa akicheza kwenye nafasi zao wakati alipotua hapa."

No comments:

Post a Comment