Friday, November 16, 2012

ALEXIS SANCHEZ NJE BARCELONA KWA MWEZI MMOJA

Alexis Sanchez

Alexis Sanchez wa Chile (kushoto) akichezewa faulo mbaya wakati wa mechi yao dhidi ya Serbia juzi.
BARCELONA, Hispania
Alexis Sánchez anakabiliwa na kipindi cha btakriban mwezi mmoja kuwa nje baada ya kuumia kifundo cha mguu wakati wa mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya timu ya nchi yake ya Chile dhidi ya Serbia nchini Uswisi juzi usiku, klabu yake ya Barcelona imesema leo.

Straika huyo mara moja alifanyiwa uchunguzi baada ya kuwasili Barcelona.

Alexis alitolewa alitolewa baada ya dakika 15 tu kufuatia faulo mbaya aliyochezewa na kiungo wa Serbia, Luka Milivojevic. Huku Sánchez akiuonekana wazi kuugulia, kocha wa Chile, Claudio Borghi hakupoteza muda kusubiri kabla ya kumtoa nyota huyo na badala yake kumuingiza Angelo Henríquez aliyecheza kwa mara ya kwanza mechi yake ya kimataifa akiwa na timu ya taifa ya wakubwa.

Kwa mujibu wa madaktari wa Barça, Alexis ameumia kifundo cha mguu wake wa kulia, hiyo ikimaanisha kwamba atakuwa nje kwa mwezi mmoja au zaidi.

Kama taarifa hizo ni sahihi, straika huyo atakosa mechi saba au nane za Barcelona, ambazo ni dhidi ya Zaragoza, Spartak Moscow, Levante, Alavés, Athletic Club, Benfica, Betis na Atlético de Madrid.

No comments:

Post a Comment