Saturday, October 6, 2012

XAVI: NITAFURAHI SANA NIKIPIGA HAT-TRICK DHIDI YA REAL

Xavi
BARCELONA, Hispania
Kiungo nyota wa Barcelona, Xavi amesema kwamba kufunga mabao matatu (hat-trick) katika mechi yao ya kesho Jumapili dhid ya mahasimu wao wa jadi, Real Madrid itakuwa ni furaha ya aina yake kwani ni ndoto itakayogeuka kuwa kweli

Nyota huyo mwenye miaka 32 ameshatwaa mataji kadhaa katika ngazi zote za klabu na timu ya taifa, lakini bado anasubiri kufunga hat-trick yake ya kwanza masihani, na anaona kuwa mechi ya kesho ya 'el clasico' itakuwa ni ndoto ya kweli pindi ikitokea akafunga kweli mabao matatu peke yake.

"Kuna kitu kingine ambacho bado sijafanya? Ni kufunga hat trick... nitafurahi sana nikipiga hat-trick yangu ya kwanza dhidi ya Real Madrid," Xavi amesema huku akitabasamu kwenye mkutano na waandishi wa habari.

"Kwakweli hatudhani kwamba ushindi dhjidi yao utazidi kuongeza migogoro ndani ya kikosi cha Real Madrid. Tumedhamiria kupata ushindi, jambo ambalo litatuongezea morari kikosini."

Kiungo huyo mchezeshaji ameendelea pia kuzungumzia hali ya majeruhi kikosini mwao kama Gerard Pique, Carles Puyol na Eric Abidal, ambaye afya yake inaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiziwa ini mwanzoni mwa mwaka huu.

"Hivi sasa, kuna nafasi ya asilimia 50 kwamba Pique atacheza dhidi ya Madrid," Xavi amesema.

"Jeraha la Puyol linasikitisha sana... yeye ni mfano ndani na nje ya uwanja kwa kila mchezaji na mara zote hucheza kwa nguvu zake zote.

"Abidal? Amehamasika sana kurejea kikosini."

Hivi sasa Barcelona wako klatika mazungumzo na wakala wa Xavi kuhusiana na mkataba wake mpya, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania anaamini kwamba makubaliano yao yanasubiri muda tu.

"Nipo katika klabu bora zaidi duniani, ningependa kustaafu nikiwa hapa. Wakala wangu anazungumza na klabu kuhusiana na mkataba mwingine mpya, hakutakuwa na tatizo lolote," amesema Xavi.

No comments:

Post a Comment