Saturday, October 13, 2012

UGANDA YAFA KIUME KWA ZAMBIA


NDOTO za Uganda kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 2013 zimezimwa jioni ya leo na mabingwa wa Afrika, Zambia kwa penalti 9-8 baada ya wenyeji kushinda mechi yao kwa goli 1-0 kwenye Uwanja wa Namboole, mjini Kigali.

Ushindi wa Uganda wa 1-0 ulifanya matokeo ya Jumla kuwa 1-1 baada ya Zambia kushinda kwa goli moja pia katika mechi yao ya awali iliyochezwa Zambia na kulazimisha mechi hiyo ichezwe kwa dakika 120.

'The Cranes' ambao hawajafungwa katika uwanja wao wa nyumbani tangu mwaka 2004, waliwapa wakati mgumu Zambia ambao walihitaji "matuta" kusonga mbele. 

No comments:

Post a Comment