Sunday, October 14, 2012

MAGOLI YA DIDIER DROGBA YAWACHANGANYA MASHABIKI WA SENEGAL... WAWASHA MOTO UWANJANI NA KUTUPA MAWE NA VYUPA WAKATI AKINA DEMBA BA WAKIWA WAMESHACHAPWA 2-0 NA IVORY COAST YA KINA DIDIER DROGBA ... MECHI YAVUNJWA, DROGBA, KOLO TOURE, YAYA, GERVINHO NA WENGINE WATOLEWA UWANJANI CHINI YA ULINZI MKALI WA 'FFU' WA WENYEJI SENEGAL

Kimenuka... Drogba akilindwa na Polisi wakati akitolewa uwanjani.
Shabiki wa Senegal akidakwa na polisi baada ya kuingia uwanjani wakati Didier Drogba (kulia) akitaka kupiga penati iliyowapa Ivory Coast uongozi wa mabao 2-0 dhidi ya Senegal katika mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2013) kwenye Uwanja wa Leopold Sedar Senghor mjini Dakar, Senegal jana, Octoba 13, 2012. (Picha: AP)
Hatari...!  Mashabiki wa 'chama' la kina Drogba wakihaha kujiokoa jana baada ya vurugu kuibuka katika mechi yao dhidi ya Senegal.

Duh...! Kimenuka hadi kitaa.... mashabiki wa Senegal wakikimbia mitaani huku wakiandamwa na mabomu ya machozi baada ya kuzuka kwa vurugu uwanjani jana.

Yaya Toure (kulia) na wachezaji wenzake wa Ivory Coast wakitolewa uwanjani na 'FFU' wa Senegal baada ya vurugu zilizotokea uwanjani jana.

Sasa uwanjani hapakaliki tena...!

Ni vurugu mtindo mmoja baada ya mashabiki wa Senegal kukasirishwa na kipigo cha Ivory Coast dhidi ya timu yao jana.

Wachezaji Ivory Coast wakitolewa uwanjani.

Wachezaji wakitolewa uwanjani wakisindikizwa na polisi baada ya mawe, chupa na vitu mbalimbali  kurushwa uwanjani na mashabiki wenye hasira wa Senegal waliokasirishwa kuona timu yao ikichapwa na kina Drogba.

Mashabiki wa Ivory Coast wakihaha kujiweka pamoja ili kujiokoa jana.Kimenuka mwanaa... hapakaliki tena uwanjani!


Kolo Toure (kushoto) akiosha mpira mbele ya nahodha wa Senegal, Pappis Demba Cisse wakati wa mechi hiyo
Yaya Toure akiwania mpira katikati ya wachezaji wa SenegalDAKAR, Senegal
Mechi muhimu ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Ivory Coast imefutwa baada ya mashabiki kuvamia uwanja mjini Dakar juzi.

Mashabiki wa wenyeji walianza kwa kuwasha moto majukwaani na kurusha mawe na vitu vingine uwanjani wakati Senegal wakiwa nyuma kwa mabao 2-0, matokeo ambayo yangewatoa katika michuano hiyo.

Mashabiki wa Ivory Coast walikimbilia uwanjani kuepuka mashambulizi.

Mashabiki na wachezaji wa Ivory Coast baadaye walitolewa nje na polisi, ambao walifyatua mabomu ya machozi kuelekea kwenye majukwaa yaliyofurika mashabiki.

Taarifa zimesema kuwa takriban watu 10 -- akiwamo Waziri wa Michezo wa Senegal, Hadji Malick Gakou -- walijeruhiwa katika vurugu hizo kwenye Uwanja wa  Leopold Sedar Senghor.

Vurugu hizo zilitokea baada ya mshambuliaji wa Ivory Coast, Didier Drogba kufunga goli lake la pili kwa njia ya penati, huku zikiwa zimebaki dakika 15 kabla mechi kumalizika. Kabla ya goli hilo la penati lililokuwa la 58 kwake kuifungia Ivory Coast, Drogba alifunga goli la kwanza katika mechi hiyo kwa njia ya 'fri-kiki'. 

Matokeo hayo yangeiwezesha Ivory Coast kuongoza kwa jumla ya mabao 6-2 baada ya kushinda pia kwa mabao 4-2 katika mechi yao ya kwanza.

"Vyakula, vinywaji na chochote kile kilichoweza kurushwa kilirushwa uwanjani, kutoka katika kona tofauti," Chris Fuglestad, mwanafunzi wa Marekani anayesoma mjini Dakar, aliiambia BBC.

Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) bado halijatoa taarifa rasmi kuhusiana na tukiuo hilo. Lakini afisa mmoja wa Senegal alikaririwa akisema kwamba sasa timu yao itafungiwa na Caf.

Wachezaji ndugu wa Manchester City, Yaya na Kolo Toure walikuwamo katika kikosi cha Ivory Coast, na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England ilisema katika taarifa yake kuwa: "Yaya na Kolo Toure wote wako salama baada ya vurugu za mashabiki kuvunja mechi wakati Senegal walipoikaribisha Ivory Coast mjini Dakar."

Vurugu hizo mjini Dakar zilifunika kufuzu kwa Ghana, Mali, Morocco, Nigeria, Tunisia na mabingwa watetezi Zambia ambao wote wametinga katika fainali hizo zitakazofanyika nchini ya Afrika Kusini Januari mwakani. Inatarajiwa kuwa Ivory Coast watapewa ushindi lakini hapakuwa na taarifa rasmi kutoka kwenye Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kwa sababu ofisi zao za Cairo zilikuwa zimefungwa. 


Vurumai hizo, ambazo zilianika tabia za soka la Afrika, zilipaka tope matukio matamu ya uwanjani katika bara lote huku Zambia wakihitaji ushindi wa "matuta" kufuzu kwenda kutetea taji lao katika fainali hizo za mwakani.

PENALTI ISHIRINI
Ilihitaji penalti 20 kabla ya Wazambia kuifunga Uganda 9-8 baada ya matokeo yao ya jumla kuwa sare ya 1-1 kufuatia kulala 1-0 jijini Kampala. 


Tunisia pia walitinga kwenye fainali hizo kwa goli la ugenini baada ya kushikiliwa kwa sare ya 0-0 dhidi ya Sierra Leone nyumbani Monastir, kufuatia sare ya 2-2 katika mechi yao ya awali mwezi uliopita. 


Youssef Al Arabi aliifungia Morocco dakika tano kabla ya mechi kumalizika, baada ya kukosa nafasi mbili za awazi, na kulipa taifa lake goli la tatu lililoamua mechi katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Msumbiji mjini Marrakesh ambako walilipa kipigo cha 2-0 walichopata katika mechi yao ya awali. 


Lakini mechi hiyo ilizungukwa na utata uliokuja katika dakika ya 60 wakato Morocco walipopewa penalti 'rahisi mno' iliyosababisha nahodha wa Msumbiji, Miro kutolewa kwa kadi nyekundu. 


Ghana walikuwa wa kwanza kufuzu baada ya kuifunga Malawi 1-0 ugenini Lilongwe na kupita kwa jumla ya magoli 3-0 shukrani kwa bao la Afriyie Acquah aliyekuwa akiichezea timu ya taifa kwa mara ya kwanza. Mali walitoa kipigo kikali cha 4-1 dhidi ya Botswana na kupita kwa jumla ya magoli 7-1 mjini Lobatse. 


Hata hivyo, walifunikwa na kipigo kizito zaidi kilichotolewa na Nigeria dhidi ya Liberia cha magoli 6-1 mjini Calabar ambapo nyota wawili wa Chelsea, Victor Moses aliyepiga mawili na John Obi Mikel 'alitupia' kwa penalti. Nigeria walifunga katika dakika kabla ya kuwang'oa wageni kwa juma la ya mabao 8-3.


Nchi ndogo ya visiwa Cape Verde iliitoa Cameroon ambayo imewahi kucheza robo fainali ya Kombe la Dunia leo na kufuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali za Mataifa ya Afrika licha ya kulala 2-1 katika mechi yao ya marudiano.

Cape Verde yenye wakazi 500,000 ilitoa pigo la kushangaza zaidi katika historia ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla ya magoli 3-2 kufuatia ushindi wao wa nyumbani wa 2-0 mwezi uliopita.

Cape Verde walitarajia kukumbana na kipigo kikali, lakini ilitangulia kupata bao katika dakika ya 22 kupitia 'fri-kiki' ya mshambuliaji anayecheza soka la kulipwa Ureno, Heldon.

Achille Emana alisawazisha dakika chache baadaye lakini walihitaji goli la dakika ya nne ya majeruhi kupata goli lao la pili kupitia kwa mtokea benchi yosso wa miaka 16, Fabrice Olinga kufuatia krosi ya Samuel Eto'o, ambalo halikuwasaidia.

Ukanda wa CECAFA ulipata mwakilishi leo baada ya Ethiopia kushinda nyumbani 2-0 dhidi ya Sudan na kupita kwa magoli ya ugenini baada ya awali kulala 5-3. 

Manucho aliifungia Angola magoli mawili katika ushindi wa 2-0 nyumbani dhidi ya Zimbabwe leo na kupita kwa faida ya goli la ugenini baada ya awali kulala 3-1.

No comments:

Post a Comment