Friday, October 12, 2012

UCHAGUZI DRFA WAAHIRISHWA

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah

UCHAGUZI wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) uliokuwa ufanyike keshokutwa Jumapili Oktoba 14, 2012 umeahirishwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, uamuzi kuhusu uchaguzi huo utatangazwa Jumanne, Oktoba 16, 2012.

Angetile amesema Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekamilisha usikilizaji rufani zilizokatwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA.

"Ili kujiridhisha kuhusu uamuzi wote uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA kuhusu waombaji uongozi wote wa DRFA waliopitishwa na ambao hawakupitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA, Kamati itatangaza uamuzi wake kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi wa DRFA siku ya Jumanne, Oktoba 16, 2012," alisema Osiah katika taarifa hiyo

No comments:

Post a Comment