Friday, October 12, 2012

TOP MODEL WA REDD'S MISS TANZANIA KUPATIKANA LEO

Baadhi ya washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012, wakifurahia kushika nyoka wakati warembo hao walipotembelea eneo la Merani Snake Park na kujionea nyoka wa aina mbalimbali, mamba, kenge, ndege aina ya bundi, tai na tumbili. Warembo hao wapo mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwaajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ikiwa ni harakati za warembo wa Miss Tanzania kila mwaka kuhamasisha utalii wa ndani.
Mshiriki wa Redds Miss Tanzania 2012, Babylove Kalala akionyesha ujasiri wa kumuuma wakati mrembo huyo na wenzake wanaowania taji hilo walipotembelea eneo la Snake Pak mjini Arusha.


Mrembo wa Kilimanjaro, Anande Raphael (kushoto) akipozi na mrembo wa Lindi, Irene Veda huku wakiwa na nyoka.wakati vimwana wanaowania taji hilo walipotembelea neo la Snake Park, Arusha.
 
Mrembo Diana Hussein alipozi na nyoka.wakati vimwana wanaowania taji hilo walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha.
 
Warembo wakimwangalia Catherine Masumbigana aliyemzungusha nyoka shingoni wakati vimwana wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha.
Mrembo wa Kitongoji cha Ukonga jijini Dar es Salaam, Mary Chizi akipozi na nyoka wakati vimwana wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha.
 
Mrembo wa Kitongoji cha Chang'ombe, Dar es Salaam Jesca Haule akisikilizia ubaridi wa nyoka wakati vimwana wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha.
 
Maweeeeeeeeeee! Mi naogopa hili jidudu.... Miss Photogenic 2012, Lucy Stephano akimwaga kilio baada ya kuvalishwa nyoka wakati vimwana wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha.

Iiiiiiiiiiiinh! mi sina urafiki na nyoka.... mrembo wa Mbeya Caren Elias akimshika kwa woga nyoka. Kulia ni Noela Michael kutoka Tabata nae akiogopa na wala hakutaka kabisa kumshika.nyoka huyo wakati vimwana wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha.

Acheni kuogopa nyoka asiye na sumu wala meno, ngojeni niwaonyeshe namna ya kupozi naye.... mrembo Lightness Michael akipozi na nyoka wakati vimwana wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha.

Mrembo wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Fina Revocatus akipozi na nyoka kwa kujiamini pamoja na wenzake wakati vimwana wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha.

 Huyo kushoto ni kama bibi wa kweli... Warembo wakiangalia sanamu ya mwanamke wa Kimasaai katika eneo la kihistoria la jamii ya Wamaasai lililopo Meserani, Arusha.

 Mrembo wa Pwani, Rose Lucas akipita katika sehemu ya Historia ya Wamasai.

Miss Tanzania 2011, Salha Israel akitoka katika vibanda vya biashara.
 
Mrembo wa Singida, Elizabeth Diamond akiangalia shanga na urembo za aina mbalimbali kwaajili ya kununua.
 
Hizi zimenivutia... Mrembo wa Kahama Mkoani Shinyanga, Happiness Rweyemamu nae alikuwa akitafuta cha kununua.
 
Mi' Mmasai bhana... Mkuu wa Itifaki ya Miss Tanzania, Albert Makoye akiwa amevalia vazi rasmi la kabila la Kimaasai akipiga picha na warembo wa Redds Miss Tanzania 2012.
 
Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye na mrembo Joyce Baluhi wakivalia mavazi rasmi ya jamii ya Wamaasai.

Na Mwandishi Wetu, Arusha
WAREMBO wanaoshiriki kuwania taji la Redd’s Miss Tanzania leo usiku wanatarajiwa kupanda jukwaani kumsaka Miss Top Model katika shindano litakalofanyika kwenye hoteli ya Naura Spring, mjini hapa.

Mrembo atakayetwaa taji hilo moja kwa moja ataingia katika 15 bora ya Redd’s Miss Tanzania katika fainali ya shindano hilo la urembo itakayofanyika Novemba 3, mwaka huu.

Mpaka sasa Miss Mbulu, Lucy Stephano amejihakikishia kuingia katika hatua hiyo, baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Miss Photogenic, lililofanyika Monduli mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana, Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Haidan Ricco alisema kila kitu kipo tayari na kinachosubiriwa ni kujua nani atatwaa taji hilo.

“Warembo wote wako sawa na wamejiandaa vema kuhakikisha wanatoa upinzani mkubwa, naamini mashabiki watakaohudhuria watapata burudani ya aina yake,” alisema.

Ricco alisema baada ya shindano hilo warembo wote wanatarajiwa kuondoka mjini hapa kesho asubuhi kuelekea Tanga kwa ajili ya kutembelea mapango ya Amboni, kabla ya kurejea Dar es Salaam.

Warembo wapatao 30 wanawania taji la Redd’s Miss Tanzania, ambalo kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

No comments:

Post a Comment