Tuesday, October 9, 2012

"TUKIMUUZA FALCAO KWA EURO MILIONI 60 MADENI YETU YOTE YATABAKI HISTORIA"

Radamel Falcao

MIGUEL Angel Gil Marin, meneja mkuu wa Atletico de Madrid, amefungua milango ya uwezekano wa kuondoka kwa straika wao Radamel Falcao mwisho wa msimu huu.

"Tukipata Euro milioni 60 kwa Falcao kutamaliza matatizo yote ya kifedha ya Atletico, madeni yetu yatabaki historia," alisema Gil.

Hata hivyo, Gil Marin alisema straika huyo Mcolombia atamaliza mkataba wake akiwa na klabu hiyo: "Hakuna shaka. Anataka kubaki, na wachezaji wote na kocha wataka abaki".

Kuhusu uwezekano wa Falcao kuhamia kwa majirani zao Real Madrid, Gil Marin alidai kuwa "kama Atletico haitafuzu kucheza Ligi ya Klabu Bingwa na itashindwa kumpatia Falcao anachokihitaji, hapo nina wasiwasi Real Madrid wataweza kumpata".

Bosi huyo wa Atletico amesema kwa machungu kwamba bodi inafanya kila iwezalo kutengeneza kikosi cha ushindani.

"Tunafanya kila tuwezacho ili kupata miujiza. Tunashindana Ulaya dhidi ya klabu zaidi ya 50 ambazo zina bajeti kubwa kuliko sisi. Tunafanya yasiyowezekana, tunachukua 'maamuzi magumu' ili kuwapa mashabiki wanachotaka. Lakini ni ngumu kuhimili," alisema.

Gil MarĂ­n pia alimsifu kocha Diego Simeone. "Kumteua 'El Cholo' (Simeone) imekuwa ni baraka kubwa kwa Atletico. Yeye ni kocha mzuri ana mahusiano mazuri na mashabiki. Wachezaji wote wanamuamini Simeone, na mashabiki wanajiona kama wako mawinguni."

No comments:

Post a Comment