Tuesday, October 9, 2012

KINYOZI AFAFANUA SABABU ZA KUMNYOA RONALDO STAILI MPYA ALIYOINYESHA WAKATI AKISHANGILIA GOLI KWENYE CLASICO

Ronaldo akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp huku alama ya "V" ikionekana juu ya sikio lake.
Vinyozi wa Ronaldo, Jose Miguel na Siero Leal
Ronaldo na staili yake mpya ya kunyoa
Refa Carlos Delgado Ferreiro akimsaidia kuinuka Cristiano Ronaldo wa Real Madrid CF wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou Oktoba 7, 2012. Timu hizo zilitoka 2-2. Magoli yote ya Real yalifungwa na Ronaldo wakati ya Barca yalifungwa na "jini" Lionel Messi.

CRISTIANO Ronaldo alimshangaza kila mmoja kwenye Uwanja wa Nou Camp Jumapili kutokana na mwonekano mpya. Ilikuwa ni staili ya nywele iliyoonyesha alama ya V. Wakati alipofunga goli la kwanza alionyesha kidole chake kwenye alama ya ushindi kichwani mwake. Kuna stori nyuma ya staili hiyo.

Mreno huyo aliwapa vinyozi ambao ni ndugu Jose Miguel na Siero Leal. Aliwaita Jumamosi na kuwaeleza kwamba anatafuta staili mpya, kitu tofauti na kitakachozua mjadala.

"Alituambia, kama ilivyo mara nyingi kwake, anahitaji kitu tofauti. Tunamfahamu vyema na tukapata wazo la kumnyoa kwa alama ambayo inamaanisha amani na utulivu ambao huupata shujaa baada ya mapambano. Alikubali," alisema mmoja wa vinyozi hao.

Kuifanya ionekane kitu kizuri ilikuwa ni jambo jepesi. Jose alisema: "Sio tu staili. Kuna sababu katika kila staili ya kunyoa. Na anahitaji staili inayoonekana. Inamfaa. Yeye ni mwenye malengo na anayependa vitu bora. Tulifanya alimbunia kilichokuwa katika hisia zake kwa wakati ule na kilionekana wakati wa mechi".

"Nywele zake ni laini sana na unapaswa kuzinyoa kwa umakini. Anapenda kuziseti ama kuzipaka mafuta mengi. Anafahamu kwamba kamera za televisheni humfuatilia kwa kila afanyalo na anapenda kuonekana mtanashati. Cristiano anajioenda sana na anapenda kutimiza malengo. Ni mshindi. Anajifikiria yeye tu," aliongeza.

No comments:

Post a Comment