Wednesday, October 17, 2012

TAZAMA JINSI KUKOSEKANA MARCELO KUTAKAVYOIATHIRI REAL MADRID... AKICHEZA USHINDI KWA REAL HUWA NI 83%, SARE 10%... AKIKOSEKANA UWEZEKANO WA REAL MADRID KUSHINDA HUSHUKA HADI ASILIMIA 61, SARE HUONGEZEKA HADI ASILIMIA 19 NA VIPIGO HUONGEZEKA HADI ASILIMIA 19

'Jembe' Marcelo akiwa kazini

Marcelo anavyoonekana leo (Oktoba 17, 2012) wakati akiendelea kuuguza jeraha la kuvunjika mguu wa kulia

Marcelo akiguza jeraha lake la mguu.
MADRID, Hispania
Kikosi cha kocha Jose Mourinho wa Real Madrid huwa hakipati matokeo mazuri kinapomkosa Marcelo. Wachambuzi wanasema kwamba Marcelo hutegemewa sana katika kuipa ushindi timu hiyo na kuielezea dhana hiyo kwa jina la utani la 'Marcelodependence'.

Ukiangalia kwa haraka takwimu za Real Madrid tangu ianze kuongozwa na José Mourinho, utagundua kwamba kweli, Marcelo amekuwa 'mhimili' wa mafanikio ya kikosi cha kocha huyo. Bila Mbrazil Marcelo, takwimu zinaonyesha kuwa mafanikio hushuka sana, na hilo ndilo linalowapa hofu mashabiki wa Real kuelekea mwanzo wa wiki mbaya za kumkosa Marcelo kwa kipindi chote atakachokuwa nje kwa miezi mitatu akiuguza jeraha la kuvunjika mguu wakati akiwa na timu yake ya taifa ya Brazil.

Katika kipindi cha Mourinho, Marcelo amecheza mechi rasmi 132, akishinda mechi mechi 110,  sare 13 na vipigo 9.

Kwa upande mwingine, Mbrazili huyo amekosa mechi 26 kutokana na kutumikia adhabu, majeraha na sababu zitokanazo na maamuzi ya kiufundi. Katika mechi hizo alizokosekana, takwimu zinaonyesha kuwa Real ilishinda mechi 16, ikapata sare 5 na kufungwa mechi 5.

Asilimia zinaonyesha wazi athari za beki huyo wa pembeni-kulia kikosini. Marcelo anapocheza, matokeo ya Real Madrid huwa kama ifuatavyo: ushindi 83% , sare 10%  na vipigo 7% .

Kinyume chake, bila ya Marcelo, takwimu hizo huwa kama ifuatavyo: ushindi 61%, sawa na punguzo la pointi 22, sare huwa 19% -- takriban mara mbili ya vile inavyokuwa pindi akicheza -- na vipigo poia huongezeka hadi 19%.

Kwa lugha nyingine, wakati Marcelo asipoichezea Real Madrid, uwezekano wa timu hiyo kufungwa huwa zaidi ya mara mbili, kutoka 7% hadi 19%. Hivyo haitashangaza kuona Mourinho akiwa katika wakati mgumu.

Mechi mbili zinakumbukwa zaidi katika misimu miwili iliyopita, ambayo Marcelo hakucheza na kuchangia mno Real Madrid kupoteza ubingwa mwaka huo: walichapwa ugenini 1-0 dhidi ya Osasuna na mechi dhidi ya Sporting ambayo walilala 0-1. Na isisahaulike vilevile kuwa Marcelo hakuwamo uwanjani wakati Real Madrid ilipodondosha pointi kwa sare ya 1-1 dhidi ya Valencia katika mechi yao ya ugenini iliyokuwa ya ufunguzi msimu huu.

No comments:

Post a Comment