Saturday, October 6, 2012

SERGIO AGUERO: LIONEL MESSI HUWA ANACHEKA SANA KILA MARA AKIKUMBUKA NILIVYOMUULIZA JINA LAKE WAKATI TUKIWA TAIFA VIJANA U-20 ARGENTINA 2005...!

Sergio Aguero (kuhoto) na Lionel Messi

Sergio Aguero
MANCHESTER, England
Sergio Aguero amefichua kwamba bado amekuwa akicheka sana na nyota wa Barcelona,  Lionel Messi baada ya kukumbuka namna alivyoshindwa kumtambua kwenye fainali za Kombe la Dunia la Vijana (U-20) Mwaka 2005 nchini Uholanzi.

Muargentina mwenzake huyo hatimaye akaibuka kuwa nyota wa fainali hizo, wakiifunga Nigeria 2-1 katika fainali.

"Tulikuwa tukizungumzia viatu, halafu baadaye akasema kitu," straika huyo katika Ligi Kuu ya England ameiambia DirectTV Sports.

"Alisema jina lake ni Lionel, nami nikamuuliza, jina la ukoo wako ni lipi? "Akasema 'Messi', na baadaye akarudia, 'Messi'. Bado sikuwa ninajua yeye ni nani. Baadaye nikasoma kuwa kuna Messi ambaye anaibukia katika timu."

Aguero aliendelea kukikiri kwamba ehabari hiyo baadaye ilikuwa chanzo cha utani miongoni mwa wachezaji wengine kikosini.

"Messi alicheka kwa furaha na bado anacheka kwa furaha wakati akikumbuka matukio haya," alisema straika huyo mwenye miaka 24, ambaye alilala chumba kimoja na mchezaji huyo aliyekuwa Mwanasoka Bora wa Dunia kwenye michuano hiyo.

"Wakatyi huo nilikuwa na miaka 17. Baadaye ilikuwa poa baina yetu."

No comments:

Post a Comment