Monday, October 1, 2012

SCHOLES, GIGGS, CARRICK, VALENCIA WOTE NJE MAN UTD UEFA KESHO

Rooney akijifua na wenzake leo

BEKI wa Manchester United, Jonny Evans atasafiri na timu kwenda Romania kwa ajili ya mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya CFR Cluj lakini Michael Carrick, Antonio Valencia, Paul Scholes na Ryan Giggs wote watakosekana katika kikosi cha Mashetani Wekundu.

Evans amekuwa na shaka ya uzima wake katika kikosi cha Sir Alex Ferguson, baada ya kutoka akichechemea mwishoni mwa mechi waliyolala 3-2 dhidi ya Tottenham Jumamosi, lakini kocha huyo Mscotland baadaye alidai kwamba beki huyo wa kati raia wa Ireland Kaskazini alipatwa na ganzi ya mguuni.

Beki huyo alifanya mazoezi leo asubuhi kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Carrington lakini Carrick na Valencia walikosa mazoezi hayo, huku Valencia akiwa pia alikosa mechi dhidi ya Spurs kutokana na majeraha ya 'enka'.

Viungo mavetarani Scholes na Giggs, hata hivyo, wanaonekana kupumzishwa licha ya Ferguson kusisitiza kwamba atachezesha kikosi chenye uzoefu.

Yosso Scott Wootton na Michael Keane walifanya mazoezi na kikosi cha kwanza leo, pamoja na beki mpya Alexander Buttner, lakini Nemanja Vidic, Chris Smalling na Phil Jones wanatarajiwa kukosekana kwa muda mrefu.

Ashley Young pia hakushiriki mazoezi ya leo lakini alijifua na makocha wa viungo mbali na wenzake wa kikosi baada ya kuumia mwishoni mwa Septemba.

Beki wa zamani wa Man United, Mikael Silvestre pia alikuwapo na akafanya mazoezi na kikosi hicho, wakati beki huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa akisaka klabu mpya baada ya
kumaliza mkataba wake na Werder Bremen. Silvestre (35) anafanya mazoezi na Mashetani Wekundu kwa ajili ya kujiweka fiti.

Kikosi cha Manchester United kilichosafiri kwenda kuwavaa CFR Cluj:

De Gea, Lindegaard, Buttner, Evans, Evra, Ferdinand, Michael Keane, Rafael, Wootton, Anderson, Cleverley, Fletcher, Lingard, Nani, Powell, Tunnicliffe, Hernandez, Kagawa, Rooney, Van Persie, Welbeck.

No comments:

Post a Comment