Monday, October 8, 2012

RONALDO ANA BAHATI MBAYA KUZALIWA KATIKA KIZAZI KIMOJA NA MESSI - VILANOVA

Lionel Messi akifunga goli la kwanza la Barcelona dhidi ya kipa wa Real Madrid Iker Casillas (kulia) wakati wa mechi yao ya kwanza ya La Liga kwenye Uwanja wa Nou Camp mjini Barcelona jana. Oktoba 7, 2012.

Lionel Messi wa Barcelona akishangilia goli lake la kwanza dhidi ya Real Madrid wakati wa mechi yao ya kwanza ya La Liga kwenye Uwanja wa Nou Camp mjini Barcelona jana. Oktoba 7, 2012.
Lionel Messi wa Barcelona akishangilia goli lake la pili dhidi ya Real Madrid wakati wa mechi yao ya kwanza ya La Liga kwenye Uwanja wa Nou Camp mjini Barcelona jana. Oktoba 7, 2012.


KOCHA wa Barcelona, Tito Vilanova amemsifu Lionel Messi baada ya kufunga mara mbili katika sare ya 2-2 dhidi ya Real Madrid jana usiku.

Cristiano Ronaldo alifunga goli la kwanza na la mwisho la mechi hiyo kwenye Uwanja wa Nou Camp, wakati Messi pia alifunga mawili huku bao lake la pili likiwa ni 'bonge' la 'fri-kiki' iliyokwenda moja kwa moja wavuni.


"Hatujui ukomo wake wa kufunga," Vilanova alisema kuhusu straika huyo Muargentina.

"Unapaswa kumuona anavyojifua mazoezini kila siku -- hilo linatufanya tuamini kwamba atazidi kutisha. Nadhani hatutaona tena mchezaji kama yeye. Yeye ni mchezaji bora aliyewaacha mbali sana wanaomfuatia." 

Vilanova aliongeza kwamba Ronaldo "angetambulika zaidi" kama asingezaliwa katika kizazi kimoja na Messi.

No comments:

Post a Comment